Wingi wa Askari Trafiki mijini ni matumizi mabaya fedha za wananchi. Wahamishwe au wapunguzwe kazi

Verily Verily

Senior Member
Jan 4, 2007
191
148
​​​Kumekuwepo na kilio cha muda mrefu kuwa idadi ya askari polisi haitoshi?jambo ambalo kweli kwa maeneo ya vijijini na miji midogo ya wilaya tu lakini sio kwenye majiji hasa Dar es Salaam na Arusha.
Hata hivyo kiuhalisia sio kweli kuwa askari polisi ni wachache bali ni migawanyo na mipangilio mibaya ya kazi.

Hivo ni vigumu kukubaliana na propaganda hizi kwa sababu zifuatazo:-

1. Katika miji mikubwa kama Dar es Salaam na Arusha utakuta askari wasiopungua watano wamesimama barabarani kila baada ya kilometa 1-3 kwa mijini na kilometa 4-5 kwenye barabara kuu ziingiazo miji mikubwa. Kwa mfanio kutoka Ubungo mpaka Chalinze kuna wastani wa askari kwenye vituo 11. Katika barabara hio utakuta hakuna njia/barabara kubwa inayoingia kutokea pembeni hivyo gari linalotoka Chalinze kuja Ubungo (and vice versa) linaweza kusimamishwa katika vituo vyote hivyo na askari wasiopungua watano. Hii ni idadi kubwa sana ya askari yaani askari 11x5=55 kazi ambayo ingefanywa kwenye vituo viwili na askari 10 makini yaani 2x5=10 , ni matumizi mabaya ya fedha kuwalipa mishahara na upotevu wa muda wa magari katika kusikmama maeneo yote 11. Idadi hii ya ukaguzi kila km1-3 huwezi kuikuta katika nchi yoyote Afrika Mashariki yamkini na nchi nyingine za Kiafrika labda katika mataifa yenye matishio ya ughaidi ambapo askari wa Jeshi la Wananchi huchukua jukumu hilo.

2. Ukaguzi unaofanya katika vituo hivyo ni Leseni, Bima na makosa madogo madogo huku vitu muhimu kama mazao ya misitu, nyara za serikali nk vikipita na kukamatiwa nje ya nchi. Hivo ukaguzi huo hauna tija ya moja kwa moja na ni ukosefu wa awajibikaji na matumizi mabaya ya mishahara na sitahili nyingine. Kwa jiji la Arusha idadi ya askari ni kubwa zaidi hata ya Dar es Salaam. Vivo hivo na kwa majiji kama Mwanza, Mbeya nk. Je uwepo wa askari wengi kama vile tuko vitani ni kwa faida ya nani au kazi ya kukusanya faini na kupunguza kuwahi kwa magari ni kwa faida ya nani?


3. Kutokana na wingi wa askari hao mabarabarani, wengine hukosa kazi ya kufanya hivo hualazimika kufanya hata kazi zenye kuleta hasara kwa uchumi wa taifa. Kwa mfano katika vituo kama Manzese Tip Top Dar es Salaam utakuta muda wa kuanzia saa 12:30-2:30 asubuhi kuna askari 2-3 wapepark gari la polisi wanaandika faini na wanazuia magari yasipite katika lane za katikati ambazo zinatarajiwa kuanza kutumika pindi mabasi yanendayo haraka yatapoanza. Muda huo ni kipindi cha ?rush hour? na lane hizo zimekamilika kwa muda mrefu zaidi ya mwaka sasa. ?Rush hour? ni wakati muhimu duniani kote ambapo watu wengi wanawahi kazini au wanatoka kazini. Majiji mengi duniani yana utaratibu wa kusaidia kupunguza msongamano ?foleni? wakati wa rush hours. Kwa Dar es Salaam,kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo mabasi ya haraka hayako barabarani na lane zake ziko tayari ni sahihi kabisa kuruhusu matumizi ya lane hizo. Foleni ya Dar es Salaam inajulikana na suala hili limejadiliwa mpaka bungeni; huligharimu taifa bil 4-5 kwa siku kwa Dar pejkee hivyo kuzuia matumizi ya lane hizi ni matumizi mabaya ya pesa za mlipa kodi. Hata hivyo barabara hizo ni mali ya wananchi zimejengwa na pesa yao.Kwa nini zizuiliwe kwa zaidi ya mwaka mzima? Tunaomba uongozi wa Jeshi la Polisi kuondoka kero hii ya kujitengenezea.

4. Wakati askari wakikosa kazi kwenye mijini, vijijini na mji midogo utakuta askari ama ni wachache ama hawapo maeneo ambayo yangestahili kuwa na kituo cha polisi. Askari waliozidi wapelekwe maeneo wanayohitajika na ambapo wataleta tija kama maeneo yenye migogoro ya wakulima na wafugaji, mikoa ya pembezoni ambapo mabasi yanatekwa na majambazi kuvamia mawananchi nk. Askari polisi wasirundikane mijini!

Rai kwa serikali yetu sikivu na yenye kusikia vilio vya wananchi wake:Moja, Ifanyike tathmini ya mahitaji ya askari polisi kwenye miji na tifa kwa ujumla na kuhamishiwa penye mahitaji. Pili, ajira ya askari wapya idhibitiwe mpaka hawa waliopo wapate kazi
 
Hawa jamaa hakuna wanalosaidia kabisa, we jiulize ni kwanini maeneo mengi hawapo badala yake wanajaa mjini. Njia ya kutoka Dom kwenda Singida kwenda Nzega na kahama ni wachache sana lakini ndo huko unakuta ajari za ajabu sana. wanataka wakae mjini wapige deiwaka zao binafsi
 


Wewe hauna Akili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…