MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 13,577
- 30,343
Nimesikitishwa sana na kitendo cha huyu msanii chipukizi anayefanya vizuri kwa sasa komredi Ali Kiba kutojua maana ya jina FALLEN ANGEL na linavyotumika. Hakuna namba yoyote unaweza kumwita binti wa beberu fallen angel akakuelewa. Mimi kama akili kubwa nitafafanua kwa maslahi mapana ya nchi.
Kwa Wakristo fallen angel ni jina alilopewa malaika aliyeasi mbinguni na kuungana na ibilisi. Walitupwa kutoka mbinguni na kuangukia duniani. Biblia inasema lile joka liliondoka mbinguni na theluthi ya malaika wote waliokuwepo. Ilikuwaje sasa Mungu wa upendo akawaacha waje duniani kutuvuruga sisi tusio na nyenzo wala mbinu zozote za kukabiliana nao? Au kwanini waasi wasingeteketezwa? Hayo maswali muulize kiongozi wako wa kiroho.
Maana nyingine ya jina FALLEN ANGEL ni mtu aliyekuwa vizuri kwa kila kitu kuanguka na kushuka thamani. Au pia biashara iliyokuwa inafanya vizuri ikaanguka. Kimsingi hakuna maana yoyote ya kupendeza kwa jina FALLEN ANGEL. Mimi siwezi kumwita mpenzi wangu FALLEN ANGEL. Ni vema watanzania tukajifunza sana kiingereza kuliko kukutana na aibu zisizo za lazima. Kutafsiri lugha ya kiingereza moja kwa moja kuja kiswahili ni upuuzi. Ukitaka kujua maana ya maneno tumia hata oxford dictionary ya english - english.
Kuhusu WIMBO NAONA NI WA HOVYO ULIO CHINI YA MATARAJIO YA WATEJA SOKONI. Ni miongoni mwa nyimbo za hovyo kwa mwaka huu. Kuna mambo mengi sana ya kiufundi yamekosekana. Msanii chipukizi Ali Kiba atafute kazi nyingine ya kufanya. Nimeuweka huo wimbo hapa ili usikilize kukubaliana nami kuwa ni wa hovyo.