BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,412
- 2,758
Ni muda muafaka sasa kuachana na malipo ya Dola ya Marekani. By William Ruto.
Rais wa Kenya, William Ruto ametoa ushauri huo kwa viongozi wa Afrika akisema ni muda wa kuanza kuchukua hatua ya kuachana na malipo ya fedha kwa kutumia Dola ya Marekani badala yake kuwepo na mfumo wa malipo wa Pan-African Payments System (PAPSS)
Amesema mfumo wa PAPSS uruhusu kufanyika malipo kwenda nje kwa kutumia fedha za ndani ya Nchi lakini thamani ya kile kinacholipiwa kinabadilika kulingana na thamani ya fedha ya sehemu husika badala ya wote kulazimika kutumia Dola
Ruto amesema “Tunapata tabu kufanya malipo ya huduma na bidhaa kwa kuwa kila nchi ina fedha zake, hatuna haja ya kuwa na Dola wala kuhamia kutumia fedha nyingine kama ya China, tukitumia PAPSS itasaidia biashara kufanyika kwa urahisi.”
Je wazo lake hili linatoa ujumbe gani kwa Marekani. Na je viongozi wenzake wa Afrika wako tayari kulipokea au bado wana akili za kikoloni kuwa wazungu ndiyo Kila kitu. Yeye Ruto kaoesha njia sasa kazi kwenu viongozi wa Afrika wapenda misaada na mikopo nafuu ya wazungu.
Sasa baada ya Rais Yowel Museven wa Uganda kupewa maua yake kwa kupitisha sheria ya marufuku ya ushoga nchini mwake, anaefuata sasa atakuwa William Ruto km viongozi wenzake watamuunga mkono.