GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,190
- 10,313
Wakati Rais akiwaapisha viongozi aliowateua, alisema aliwaacha Kabudi na Lukuvi kwa lengo la kuwavuta jirani naye kwa lengo la kumsaidia kazi maalum Ikulu.
Ilionekana kama hayo majukumu yangekuwa mazito zaidi na ya heshima zaidi kuzidi ya uwaziri. Hii ni kwa sababu walikuwa wawe "viranja" wa mawaziri!
Miaka miwili imeshapita tokea Rais aliseme hilo, 2022. Lakini hao "waheshimiwa" wamekuwa kama vile "wamepotea" kwenye medani za kisiasa. Hawasikiki tena! Ni afadhali na walivyokuwa mawaziri.
1. Ni kweli majukumu yao kwa sasa ni ya kuwasimamia mawaziri?
2. Hayo majukumu yanamnufaisha nani? Taifa? Rais? Wanasiasa? Wao binafsi?
3. Wao binafsi wananufaikaje na hizo nyadhifa mpya zisizotambulika kikatiba?
4. Kukubali kwao hayo majukumu mapya ambayo yamewafanya wasiwe wanasikika sana kama walivyokuwa mawaziri si sawa na "kujinyonga" kisiasa?