Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 552
- 1,517
Wakuu,
Inaonekana mambo yanazidi kutokota ndani vya CHADEMA kadri siku zinavyozidi kwenda.
Hivi karibuni, Dk. Slaa ameonyesha kukerwa na ukimya wa CHADEMA kuhusu tuhuma za rushwa zilizotolewa na Tundu Lissu, makamu mwenyekiti wa chama hicho.
Ikumbukwe kuwa miezi chache nyuma Tundu Lissu akizungumza katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse alinukuliwa akisema
"Kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi, yeyote anayesema hakuna tatizo anatudanganya, kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi na rushwa ya uchaguzi ya mtu yeyote yule ni adui wa demokrasia na ni adui wa haki, kiongozi yeyote anayepatikana kwa kununua wapiga kura huwauza siku ikifika, kwa hiyo nilichokisema Iringa ninakisimamia kama nilivyokisema, kuna tatizo la rushwa linatuvuruga CHADEMA.
Dkt Slaa amesema kuwa, Lissu, akiwa katika nafasi ya uongozi wa juu, alikuwa na nafasi ya kutumia mamlaka yake kuhakikisha kwamba tuhuma hizi zinajadiliwa kwa kina ndani ya chama na kufanyiwa kazi ili ukweli ujulikane.
Soma pia: Tundu Lissu: Kuna Rushwa inatuvuruga ndani ya CHADEMA
Hata hivyo, Dk. Slaa ameonyesha masikitiko kwamba badala ya kuanzisha mjadala wa ndani ambao ungetafuta ukweli na kutoa majibu kwa umma, CHADEMA imechagua kukaa kimya, hali ambayo inaacha maswali mengi kwa wanachama na wafuasi wa chama hicho.