Wilaya ya Mbarali (Tanesco) inaongoza ukataji wa umeme Tanzania!

Action and Reaction

JF-Expert Member
Oct 16, 2021
1,431
1,484
Ni kweli kwamba kuna shida ya umeme Tanzania ila wilaya hii inaongoza kwa kukatiwa umeme, unaweza kuona siku nzima hakuna umeme au umeme unaletwa usiku wa manane nao sio zaidi ya masaa matatu au manne.

Kinachonishangaza halmashauri ya Makambako na Mbeya mjini umeme unakuwepo but hii halmashauri ya katikati umeme hakuna!

Mbarali no halmashauri yenye mashine nyingi za mpunga na kutokana na joto wananchi hutumia maftiji kuhifadhi vinywaji lakini kwa Sasa hakuna maana ya kupelekewa umeme vijijini!

Baada ya kufanya uchunguzi nimegundua:
1) Kuna watu (Waburushi) wanafanya biashara ya majenereta na Sola hivyo wanakula njama na TANESCO ili umeme ukatwekatwe wauze bidhaa zao.

2) Watanzania wengi hawana uwezo wa kununua majenerator yao hivyo inapelekea wengi wao kukaa Giza!

3) Viongozi wengi wa kiserikali na kichama ni wakulima wakubwa awe mwenyekiti wa jitongoji, Kijiji au wa chama au diwani. Hivyo hawana habari na wananchi juu ya ukataji wa umeme kwani wao hutumia majenereta!

Wito wangu Mbunge wa Mbarali Mhe. Ndingo uliishinda kwa kishindo ili uwapiganie watu wako hivyo unawajibu wa kufuatilia hili swala la ukataji wa umeme siku nzima wakipendelewa masaa matatu 3 au manner 4 kwa siku Tena usiku wa manane!

Katibu mwenezi wa CCM alisema niwakati wa kudeal na wakata umeme tena kwa makusudi! Naomba msikie makelele yetu Wana Mbarali!

Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko watanzania tunaoishi Mbarali tunaomba ukataji wa umeme uwe sawa na wilaya nyingine na sio kwa utaratibu kama huu unaofanywa na huyu manager tanesco Mbarali! TANESCO Mbarali imejaa rushwa!

Mama Samia wewe ndio rais wetu hivyo tunaomba msaada maana umeme uliwaka kwa starehe wiki la mwengu tu!
 
We jamaa unasema nn. Huku kwetu kuna waya wa TANESCO ulikatika ukawa chini week nzima hakuna aliedhurika. Na wananchi hawajali.
 
Back
Top Bottom