Wiki ngumu sana kwa Mamelodi na Al Ahly Kwa kile watakachokutana nacho kwenye dimba la Benjamin Mkapa

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
391
1,168
Wiki inayoanza kesho ni wiki ngumu sana Mamelodi na Al Ahly Kwa kile watakachokutana nacho kwenye dimba la Benjamin Mkapa dimba ambalo Yanga SC na Simba SC wamezoea kufanya mabalaa Kwa kila mgeni anaekanyaga kwenye ardhi ya Tanzania.

Najivuniaa Simba SC na Yanga SC kwenye miaka ya karibuni namna wanavyouheshimisja uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya wageni.

Msimu huu Yanga SC wamewafanya kitu mbaya CR Beloiuzdad na Medeama wakati Al Ahly walipata sare na haikuwa kinyonge msimu uliopita kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho hakuna mpinzani wa wananchi ambaye hakumbuki wakati mgumu aliokutana nao kwenye Estadio de Benjamin Mkapa.

Simba SC Kwa miaka kadhaa sasa wameufanya uwanja huu kuwa machinjio dhidi ya wageni sio kutoka Kaskazini mwa Afrika Magharibi, Kusini Wala ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati anaependa kukutana na Simba SC kwenye dimba la Mkapa na msimu huu Wydad na Jwaneng Galaxy wamekufa Kwa Mkapa huku ASEC Mimosas akiondoka na sare.

Hata National Al Ahly anajua ugumu wa kupata matokeo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa hasa anapokutana dhidi ya Simba SC ambapo katika mara tatu za mwisho walizokutana waarabuu hao wamepoteana mara mbili wakipata mara moja.

Ijumaa na jumamosi shughuli nzito zitafanyika kwenye dimba la Benjamin Mkapa na Mamelodi Sundowns na Al Ahly wataenda kuhadithia makwao
 
Attachments

  • Screenshot_20240313-073207.png
    Screenshot_20240313-073207.png
    392.9 KB · Views: 3

football sio siasa
 
Back
Top Bottom