VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,904
Mwaka 2010, Tundu Lissu aligombea kwa mara ya kwanza nafasi ya ubunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA akiwa na umri wa miaka 42. Mgombea wa Urais wa CHADEMA alikuwa Dr. Wilbrod Slaa na huku wa CCM akiwa ni Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa kauli yake mwenyewe, tena akiwa anatetea urais wake, Kikwete alikaririwa akisema kuwa ni heri dr. Slaa awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuliko Lissu kuwa Mbunge. Lissu akatoboa. Akauwasha moto mkali sana Bungeni. Why always Lissu?
Mwaka 2017, Lissu alitangaza kugombea urais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS). Ikawa nongwa. CCM na Serikali tukajipanga na kupangika katika kumzuia asishinde Urais wa TLS. Tukawasukumia makada wakuda kwenye kugombea naye. Uwekezaji na nguvu kubwa vilitumika kumzuia. Akatoboa. Lakini hakumaliza uongozi wake.
Katika kumzuia Lissu na yeyote wa aina yake kuwa Rais wa TLS, yakafanyika mabadiliko ya sheria zinazoratibu TLS. Wanasiasa na watumishi wa umma wakazuiwa kisheria kugombea. Wakiwa wa CCM, huwa wanagombea lakini kutoboa huwa ngumu kama njumu.
Mwaka huo huo 2017, mwezi Septemba, Lissu alitoa hoja za haja Bungeni akipinga na kukosoa kwa ajili ya kurekebishwa mikataba mbalimbali ya kimataifa na sheria zinazohusu rasilimali asili za Tanzania. Hoja zake hazikupendwa. Alipotoka tu Bungeni wakati wa mapumziko ya mchana, akashambuliwa kwa nia ya kuuliwa. Akatoboa na amezidi 'kupoa'.
Mwaka huu, Lissu ametangaza na ameshajaza fomu za kugombea Uenyekiti wa CHADEMA. CCM na Serikali yetu imetubidi tubadili gia angani. Tumeugeuka msimamo na masimango yetu kwa Mbowe kubaki Mwenyekiti wa CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20. Waziwazi, tunamuunga mkono Mbowe ili aendelee kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Kisa ni Lissu. Lazima azuiliwe asiwe Mwenyekiti.
Kwanini Lissu anaogopwa kwa kiasi hiki na CCM na Serikali yake? Ana upekee gani? Kwanini upekee huo wa Lissu usitumike kwa manufaa ya taifa letu la Tanzania?
Why always Tundu Antiphas Mughwai Lissu?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Masasi, Mtwara)