Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 416
Programu tumishi ya mawasiliano ya Whatsapp haitafanya kazi katika baadhi ya simu kuanzia mwaka 2021, baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti.
Programu hiyo haitafanya kazi katika simu za Android zinazotumia toleo la 4.0.2 au ndogo zaidi ya hiyo, na kwa simu za iPhone zinazotumia toleo la 9 (iOS 9).
Kwa watumiaji wa simu za 4S, 5, 5S, 5C, 6 na 6S watatakiwa kuhakikisha wanatumia toleo la iOS 9 au jipya zaidi ili kuweza kuendelea kutumia app hii maarufu ya mawasiliano.
Bonyeza Settings > General > Information
Hapo utaona kuhusu taarifa za toleo la programu endeshaji yako.
Android:
Bonyeza Settings > About System/Device
Kama utaona toleo unalotumia kwenye simu yako ni kati ya matoleo tuliyoyataja kwamba hayatakuwa na uwezo wa kutumia app ya WhatsApp tena basi hakikisha unasasisha/update.
Programu hiyo haitafanya kazi katika simu za Android zinazotumia toleo la 4.0.2 au ndogo zaidi ya hiyo, na kwa simu za iPhone zinazotumia toleo la 9 (iOS 9).
Kwa simu za Android
Kama simu unayotumia ina toleo la Android la 4.0.2 na nyuma basi itakuwa ndio mwisho wa kuweza kutumia app ya WhatsApp. Simu ambazo hazina uwezo wa kupata toleo la Android la juu zaidi ya hapo ni pamoja na HTC Desire, Motorola Droid Razr, na Samsung Galaxy S2. Simu hizi hazitakuwa na uwezo tena wa kutumia WhatsApp.Kwa iPhones
Simu za iPhone zinazotumia programu endeshaji ya iOS ya chini ya toleo la 9 (iOS 9) zote zitakosa kupata app ya WhatsApp tena. Kwa sasa hii ina maanisha simu za iPhone 4 na nyingine zote zilizotoka kabla yake.Kwa watumiaji wa simu za 4S, 5, 5S, 5C, 6 na 6S watatakiwa kuhakikisha wanatumia toleo la iOS 9 au jipya zaidi ili kuweza kuendelea kutumia app hii maarufu ya mawasiliano.
Ili kuangalia toleo la programu endeshaji la simu yako na ikiwa simu yako itaweza kutumia WhatsApp:
iPhone:Bonyeza Settings > General > Information