Hili la Dollor limeniuzi saaana. Last week nilikuwa nafanya manunuzi mtandaoni nilitamani nipasuke. Sijui tunaelekea wapi, shillingi inazidi kudolola tuuu...
Ndio utasikia Watu wanasema hapa kazi tu, dah inauzi sana. Mfumuko wa Bei ndio usiseme, jamaniiii
Unafahamu falsafa ya ukapa?
Wakati Mkapa "alitangazwa" na NEC kuwa ndio Rais wa Tanzania, si unaelewa kazi ya NEC? hii hali ya ukapa ilitokea. Che Mkapa aliondoa hela kutoka mifukoni na mikononi mwa watanuzi,watumiaji wa mtaani na kupelekea watu kuisoma namba.
Namba itasomeka zaidi kwa muda halafu uzalendo utazidi ,sambamba na upunguzaji wa deni la taifa, kulipa madeni.Ndio tutalipa madeni kwanza ili tusifiwe na wadeni wetu na tukopesheke.
Msisahau Magu ni CCM. Chama cha jembe na NYUNDO.
Ukipigwa kibao shavu la kushoto, geuza na la kulia.
Hapana kazitu.
Wadanganyika bana ni watu wa ajabu. Mlisema mnata Raisi "dikteta" sasa wacha tufaidi udikiteta na udaktari wa kutumbua majipu. Namba itasomeka tu.
X zimeanzia kwenye nyumba na majengo, baadae watu pia watawekewa X...ni kusoma namba mbele kwa mbele.
Ili nchi iwe ya viwanda ni lazima siri-kali imuondolee mwananchi uwezo wa kifedha ili bidhaa zitakazozalishwa kwenye hivyo viwanda zisafirishwe nje ili nchji ipate maduhuri ya kutoa elimu ya msingi bure na uwezo wa kununua tingatinga zaidi ili kusafisha miji. Maisha ya mjini yakimshindeni hamia kwa kijiji.
Tinga tinga zitakapomaliza kazi za usafi wa mijini zinapelekwa vijijini ili kuwasaidia wanakijiji na wakulima katika shughuli za kilimo. Kilimo pia ni viwanda na wengi watapata ajira huko.