Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 36,176
- 41,189
Ujumbe huu ni kwa wewe askari uliyezimikiwa bodaboda yako mchana maeneo ya 88 Gloness Morogoro leo mchana, ulijua kabisa chombo chako hakina mafuta ya kutosha still ukaingia nacho barabarani, kimekatikiwa mafuta ukagandisha nacho barabarani ati hata wenye magari wakupishe, baada ya honi kuzidi ukashuka na kuanza kusukuma kisha ukakidandia na kuserereka nacho kuelekea kituo cha mafuta.
Sawa hukutaka kuumbuka lakini hukutumia busara, umefika kituo cha mafuta ukawataka wakuwekee mafuta, wakakuwekea baadaye ukajipapasa mfukoni ukashtuka kama vile umeibiwa pesa, ukataka kuondoka ati wauzaji wasubiri ukawachukulie fedha kama vile wanakujua.
Lakini bahati nzuri wauzaji wa mafuta walikukomalia ukabakisha chombo kijidhamini wewe ukaenda pembeni kuwapigia jamaa zako wakutumie fedha ili ukomboe chombo pale petrol station, nashauri askari unapokua umekwama tumia busara badala ya ubabe ujuaji na nguvu ili kulinda heshima yako na jeshi lako.