Western Union tatizo liko wapi?

Powder

JF-Expert Member
Jan 6, 2016
4,800
6,294
Wakuu nimetumiwa pesa toka Europe, natumia majina 3, nimeenda Bank ya Posta wananambia Jina langu linasomeka tofauti kwenye System Yao, tofauti Na kwenye kitambulisho, kwamba jina la mwisho ambalo Ni la ukoo lipo Kati, Na la Kati lipo mwisho, Cha ajabu Sender alinitumia form yake, inasoma majina yangu sawa Na kitambulisho changu, sasa najiuliza tatizo liko wapi? Last time nilitumiwa pesa nyingine Na the same Client, nlianzia Bank hiyo hiyo ya Posta, wakakataa kunipa pesa, nikaenda Azania Bank wakanipa pesa, ila Teller akanambia next time mwambie Sender aandike majina yako Kama yalivyo, Leo nimeenda Azania wanasema Ni wiki sasa Network iko down, Posta Bank ndo hawataki hata kunisikiliza, Nimecheki Na Sender akawasiliana Na Western Union huko kwao wanasema Majina yangu yapo sawa Kama Yanavyoonekana kwenye form walionitumia, (Wanasema tatizo litakua Tanzania), System za wabongo zinasema majina yangu yamechanganywa, la Kati liko mwisho Na mwisho Kati, tatizo liko wapi? Kuna yoyote mwenye uzoefu Na kilichonikuta?

NB:Nasikitika Sana kwa kukosekana huduma ya PayPal hapa, Mimi nauza kazi zangu ulaya, sometimes client hawapendi kutumia njia ya Bank, wanataka PayPal, nawaambia nchi hairuhusu PayPal, nawaomba watume pesa kwa Western Union, Na kwenyewe Inakua usumbufu, tena nianze kumwambia Client aende kwenye office alotuma pesa kuhakiki, wenzetu hawapendi usumbufu, next time hawezi kufanya biashara Na Mimi tena!.....
 
Pole sana,ngoja nisubiri wajuzi waje,ila ninachojua ni wasumbufu sana ikiwa majina yatachanganywa,ninachokushauri kila mteja wako mtumie copy ya kitambulisho chako ili aandike majina yako kama kitambulisho kilivyo!
 
Siku nyingine waambie watumie world remit, iko bomba na reliable. western union ni kampuni inayoelekea kufa. Matawi mengi europe wamefunga, hivyo wakati mwingine wanafanya unoko ili hela yako waizungushe.
 
Asante Mkuu! Sender kaandika majina yangu sahihi kabisa, Na kanitumia copy ya form Majina yapo sahihi, lakini hapa Bongo wanasema yamekosewa, nawaonyesha form ambayo majina yangu yapo sahihi, wanasema Wao waangalia System Yao. Sasa najiuliza majina yanabadilika wapi?
 
Siku nyingine waambie watumie world remit, iko bomba na reliable. western union ni kampuni inayoelekea kufa. Matawi mengi europe wamefunga, hivyo wakati mwingine wanafanya unoko ili hela yako waizungushe.
Hii World remit inafanyaje kazi mkuu? Ni the same Kama Western Union?
 
Mwambie ndugu yako arudishiwe hela yako then tumua WORLDREMIT. hapo hela zako zinaingia direct kwenye tigo au m- pesa. Hutapata usumbufu wa kukaa kwenye foleni. Hua natumia sana hi worldremit
 
Mwambie ndugu yako arudishiwe hela yako then tumua WORLDREMIT. hapo hela zako zinaingia direct kwenye tigo au m- pesa. Hutapata usumbufu wa kukaa kwenye foleni. Hua natumia sana hi worldremit
Inafanyaje kazi hii Mkuu! Ili nimshawishi? Yeye Ni mteja wa bidhaa zangu! Anatumaje pesa?
 
Inafanyaje kazi hii Mkuu! Ili nimshawishi? Yeye Ni mteja wa bidhaa zangu! Anatumaje pesa?

Kwanza inabidi awe na credit card, visa mastercard. Then ata fanya registration kwenye website Yao, anafungua account.then ni kufuata maelezo kwenye website Yao jinsi ya kutuma. Ni rahisi sana
 
Kwanza inabidi awe na credit card, visa mastercard. Then ata fanya registration kwenye website Yao, anafungua account.then ni kufuata maelezo kwenye website Yao jinsi ya kutuma. Ni rahisi sana
Ok, nimekusoma mkuu, nashukuru Sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…