Wazungu wanavyothamini Mbwa kuliko binadamu wenzao, chanzo ni nini hasa

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
19,168
35,804
Jinsi wazungu wanavyowajali Mbwa wanaowamiliki, wakati mwingine ni zaidi wanavyojali binadamu wenzao.

Mtu anaweza asiwe anaishi na binadamu mwenzie, lakini anaishi na Mbwa ambaye bajeti yake ya kumtunza inazidi gharama za kuhudumia binadamu maskini walioko mtaani.

Huwa najiuliza chanzo cha wazungu kuwajali kiasi hiki Mbwa kuliko binadamu wenzao, sipati jibu.
 
Sidhani kama ni kweli wanajali wanyama kuliko binadamu.
Ila kwa uwelewa wangu wa kawaida nadhani sababu ni kwamba binadamu wa sasa wanaogopana.
Kwa nini binadamu wa sasa wanaogopana?
1.Hawana shukrani
2.Hawaridhiki
3.Wana wivu na chuki
4.Wana tamaa
5.Wana lawama
Sasa ukiona mtu anaishi na mnyama tu kwenye nyumba yake jua kwamba anaogopa walimwengu huenda alishawahi kutendwa akapata fundisho.
Wewe hujawahi kuona mtu unamsaidia kwa wema tu kisha baadae anageuka na kuwa adui yako.
Au umemsaidia mtu hifadhi ya kuishi kisha baadae anajisahau na kuona yupo kwake hadi mnapelekana mahakamani.
Unaweza kumsaidia mtu chakula kisha baadae anakugeuka na kukwambia ulimuwekea sumu kwenye chakula akadhurika na watu wanaosikia wataamini ni kweli.
Ndio maana mtu kuondoa hizo purukushani anaona bora akae na mnyama ili kujiweka bize kupunguza upweke.
Ogopa sana kiumbe kinaitwa binadamu ni zaidi ya simba akikuamulia jambo lake
 
Jinsi wazungu wanavyowajali Mbwa wanaowamiliki, wakati mwingine ni zaidi wanavyojali binadamu wenzao.

Mtu anaweza asiwe anaishi na binadamu mwenzie, lakini anaishi na Mbwa ambaye bajeti yake ya kumtunza inazidi gharama za kuhudumia binadamu maskini walioko mtaani.

Huwa najiuliza chanzo cha wazungu kuwajali kiasi hiki Mbwa kuliko binadamu wenzao, sipati jibu.
Mbwa wana shukrani na utu kuliko watu.
Mbea wana utu sana lakini watu wamekuwa maumbwa.
 
Usaliti, wivu uliopitiliza, kisasi kwenye mambo madogo, ugomvi unaoleta uadui mtu anajionea bora kujifugia kajimbwa kake.

Binafsi napenda Mbwa, ila siwezi ishi na Mbwa tu ndani, lazima binadamu wawepo tuparuane tu hamna shida.
 
IMG_20230426_2953.jpg
 
Aisee!!

Mbwa wamekuwa watu na watu wamekuwa Mbwa...😛😛😛
Watu wanajisahau sana, wanadhani they are irreplaceable. Wanatakiea wapigania sana hadi yao badala ya kudhani haiwezi kupotea au kuwa replaced. Sasa hivi wanyama ni trainable, robots nao ndiyo hao wanatengenezwa kuweza ku fit kwenye hadi shughuli za kiasili za nyama kwa nyama.
Unakita jitu na maumalaya yake nyeti zinajua kila aina ya uume eti na yeye anajiona ni irreplaceable anadai ladha ya mtu ni ya mtu tu tofauti na robot, uaani ana amini analishinda robot.
Watu wanapaswa kuutafuta sana utu, bahati mbaya hawajui utu unafananaje, ila sasa hivi ukitaka kujifunza utu basi kuwa karibu na wanyama
 
unaangalia mambo kijuu juu sana kama wangethamini mbwa klk binadamu wangekuwa na njaa kama tanzagiza, wangekuwa na watoto mitaani wakipekuwa majalalani kutafuta chakula kama tanzagiza, bajeti ya tanzagiza karibia nusu inatoka kwa Christian Wazungu unaosema wanathamini mbwa bila ya msaada wa Mzungu Christian sidhani kama leo hii ungejua kusoma na kuandika labda ungekuwa unajua kunrecite kuran tu, isotoshe kama Wazungu wanathamini mbwa klk binadamu na wewe na tanzagiza mnathamini nini ?
 
Acha jazba.

Kwenye tafiti zao wenyewe inaonesha watu wanawaamini zaidi Mbwa kuliko binadamu wenzao.

Hayo mambo ya njaa ni nje ya mahusiano. Kutusaidia haimaanishi wanatupenda.

kuna uhusiano wa moja kwa moja, kama wangejali mbwa klk bindamu ina maana binadamu wasio na uwezo huko wangedharauliwa na kufa kwa njaa kama tanzagiza, watoto wangelala nje mitaani kwenye maboksi kama tanzagiza, wamama wangejifungulia nje, jamii ambayo watoto hawaendi shuleni wanachunga ng‘ombe au mtoto wa miaka 12 kuolewa na babu ndiyo ambayo inajali mbwa klk binadamu, isitoshe tanzagiza ni bora uuwe binadamu klk uguse mnyama wa hifadhi unajua ni kwa nini ? nani sasa anayejali mnyama klk binadamu ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom