Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,285
- 22,948
Katiba Bora ni kitu muhimu, hilo halina mjadala na ubishi. Lakini mwisho wa siku kama wanaoisimamia hiyo 'Katiba Bora' ni wezi, wachumia matumbo, majitu yenye ubinafsi uliokithiri na wasiokuwa na uzalendo; basi Katiba bora yo yote huwa ni bure ghali.
Rais Magufuli, Rais wa tano wa Tanzania, alileta miradi mikubwa sana ya maendeleo katika muda miaka mitano kuliko Rais mwingine yoyote tangu nchi yetu ipate uhuru. Lakini hakutumia Katiba Mpya.
Rais Ibrahim Traore hivi sasa ndiye Rais bora kuliko wengine wote katika bara la Afrika. Lakini kipaumbele chake hakikuwa Katiba Mpya, bali *uthibiti wa wezi wa mali ya umma wa ndani na wa nje ya nchi yake." Mafanikio ya maendeleo nchini Burkina Faso hivi sasa yanaonekana kama ni miujuza, lakini hakuna muujiza wowote, yote anayoyafanya Rais Traore ni ya kibinadamu, na yote yanaigika.Viongozi wetu waige anayofanya Rais Traore,watakuwa wanatutendea haki na tutawapenda kama anavyopendwa Rais Ibrahim Traore na wananchi wake..Vinginevyo wataendelea kuwa maadui WA Watanzania.