Tumeweka mikakati kwa muda mrefu sana juu ya suala la kikimo bila mafanikio makubwa katika eneo hilo.
Kila mwaka au pengine kila uchaguzi tumekuwa tunasema na kupanga kuhusu kukipa kipaumbele Kilimo nadhani toka enzi za kupata uhuru bila kuwa na mafanikio.
Tumejionea viongozi wastaafu wakuu wa nchi hii wakituonesha mafanikio makubwa kwenye kilimo.
Mifano miwili na muhimu ni viongozi wakuu wa serikali ya awamu iliyopita mheshimiwa Pinda kwenye shamba lake la Nyuki na Mheshimiwa Kikwete kwenye shamba lake la mahindi.
Haya ni mafanikio na ishara ya kipekee.
Hoja yangu:
Ili kuhakikisha Kilimo kinasonga mbele ni lazima kama nchi tufanye jambo la ajabu...
Serikali na bunge wapitishe sheria ya kwamba kila kiongozi wa kisiasa wa ngazi za juu mfano kuanzia ubunge na uwaziri ni lazima amiliki shamba kubwa la mfano la kilimo.
naamini kwa kufanya hivi tutakuwa na mashamba kadhhaa ya mfano katika kila kona ya nchi...ambayo yataajiri na kuendeleza elimu ya kilimo.
naamini pia kwa njia hii viongozi wetu watahakikisha sera hii ya kuendeleza kilimo inatekelezwa kikamilifu.