Waziri wa Viwanda: Tumeongeza kodi kwenye mitumba na itapigwa marufuku ndani ya miaka mitatu

binafsi niko kwenye industry ya ushonaji,anacho kizungumza waziri ni ndoto za mchana hayo kutokea ndani ya miaka mitatu,mfano mpaka sasa hapa bongo kupata materials nzuri za kutengeneza mashati ni mtihani chaguo ni batiki,kitenge au bazee nazo hizo zilizo quality zazima uagize inchi za afrika magharibi.zeo hii vitenge vinavyo zalishwa hapa ndani havina soko kwa wavaaji wa kisasa bado viwanda vyetu vinafikiria kua tupo enzi za mwalimu so mavitenge yao yapoyapo tuu.Hata materials za kushona suti au salawili(suluali) bongo hii hakuna vyote vina toka njee,sasa waziri anayo sema sijui ana muujiza gani atao kuja nao.

Hata technology zetu bado sanaaa wakati sisi kwenye viwanda vye bado tuna weka vifungo kwa mikono wenzetu wana computerized machine ambazo zina weka vifungo,zina piga pasi,zina kagua nguo kua iko kama ilivyo kusudiwa.kama niko sahihi chu kikuu cha UD ndo pekee kina toa degree ya textile technology kwa hapa tanzania,na nadhani mwaka huu ndo batch ya kwanza tangu kuanzishwa kozi hii wanamaliza.ingekua bora kama waziri ange wekeza kwanza huku kwenye textile technology halafu ndo akaja na hayo matamko.
 
Tunapiga marufuku mitumba inayoagizwa nje ya nchi na tunaruhusu nguo mpya zinazo agizwa nje ya nchi vilevile, kwa maana nyingine nchi itatumia dola nyingi zaidi katika sekta ya nguo ukilinganisha na hapo awali, nawasiwasi na weledi wa huyu waziri,
 
Hivi hizo nguo za viwandani (Tz) zitakuwaje kuwaje?
Najaribu kuvuta picha...
Zitakuwa zinauzwa madukani au kama mitumbani?
Kwanza wote mtakuwa mnavaa batiki ndo litakuwa vazi kali sana. Wale wasiokuwa na uwezo kama yule jirani yako ataanza kuvaa kaniki, ila sasa wakazi wa Dar kaniki na joto ndo mtakoma!
 

Hayo ni mawazo yako. Viongozi walioko madarakani walishakwambia wale waliokuwa wanaishi kama malaika itabidi waishi kama mashetani. Kauli hii ukiitafakari vizuri ni kauli inayoleta mabadiliko makubwa ... na kumbuka mabadiliko makubwa sio kwamba lazima yawe mazuri ..
Mfano: Waliokuwa wanapendelea kufanya manunuzi nje ya Afrika, wataanza kubaki hapa Afrika.
Waliokuwa wanapendelea manunuzi ya hapa Afrika, / Tanzania hawatakuwa na uwezo huo na badala yake maisha yatakuwa bora liende tu
 
Bora wewe uliye kwenye Textile Industry umewapasha ukweli kuwa it is a day dream kusema within 3 years nchi itapiga marufuku uagizaji wa mitumba na nguo brand new kutoka nje ya nchi. na viwanda vyetu nchini vikawa na uwezo wa kuwavalisha watanzania milioni 45!
 
It is true.

Naona azma ya serikali ya Magu ni kuhakikisha majority ya watanzania wanaishi kama mashetani...

Except wao Watawala ndiyo waishi kama Malaika.... .
 
Alisema alichaguliwa na masikini ili awasaidie, sasa wataisoma namba
Tena wananchi wataisoma namba kwa spidi ya mwendokasi....

Tumeanza na kununua sukari kwa mwendo wa kupaa sasa inakuja kuvaa uniform kwa nchi nzima kwa mavazi ya batiki na vitenge vya Urafiki....
 
Kama hao watendaji wa serikali ya awamu ya 5 wanafanya maamuzi ya kukurupuka wakiamini kuwa ndiyo wanamfurahisha Mfalme, lakini watambue on other side of the coin wanatukomoa sisi wananchi masikini.....
 
It is true.

Naona azma ya serikali ya Magu ni kuhakikisha majority ya watanzania wanaishi kama mashetani...

Except wao Watawala ndiyo waishi kama Malaika.... .
Daima anasema nitahakikisha wastaafu wanaishi vizuri, ambao hao ndo wametufikisha hapa. Anafanya hivyo ili naye akifikia wakati wa kustaafu alindwe - asiguswe kwa mabaya atakayokuwa amewatendea watanzania.

Asiyesikia la Mkuu ...

Tulisema sana hapa kwamba tatizo la Tanzania ni mfumo mbovu ulioko ndani ya ccm, sasa tuloyasema yanatimia. Mfumo usiofaa hauwezi kukukwamua kutoka kwenye shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…