Sasa ukisikia maamuzi ya kukurupuka ya serikali ya awamu ya 5, basi ni haya ya design hii.
Sisi wananchi masikini tumekuwa kwa miaka mingi tikiponea kwenye mavazi ya mitumba.
Wala huyo Waziri wa viwanda asitake kuudanganya Umma wa watanzania kuwa within 3 years nchi itakuwa na viwanda vya nguo vya kuwavalisha watu milioni 45!
Pia ni dhahiri kwa mwendo huu wa serikali ya awamu ya 5 kufikia azma ya nchi ya viwanda ni sawasawa na 'daydream'
Inawezekana sasa serikali ya awamu ya 5 inataka kutimiza azma yao kubwa iliyojificha 'under the carpet' za kutaka kila mtu aishi kama shetani, na watanzania kwa mamilioni waanze kutembea uchi mabarabarani....
Naweza kudiriki kuiita hiyo kauli ya kuwa within 3 years kutapigwa marufuku ya kuingiza nguo za aina yote ya mitumba kuwa ni mawazo purely ya kishetani!