Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,060
- 708
WAZIRI WA ULINZI NA JKT AZINDUA BOMU BARIDI LA KUFUKUZA TEMBO
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 13 Mei, 2024 jijini Dodoma amezindua Bomu baridi la kufukuza tembo katika maeneo ya makazi na karibu na hifadhi kwa kusema ugunduzi wa bomu utakuwa ni suluhisho ya kutatua changamoto za uvamizi wa tembo katika makazi ya wananchi.
Uvumbuzi wa bomu hili baridi umekuja kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 20 Septemba, 2023 alilotoa akiwa katika ziara ya uwekaji jiwe la msingi katika hospitali ya Mitwelo mkoani Lindi, alisema Serikali yake inaendelea na jitihada za kutatua changamoto ya tembo kuvamia makazi na kuhatarisha usalama wa watu ikiwemo kuharibu mazao hususan katika mikoa ya Lindi, Arusha, Manyara, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro na Simiyu. Hivyo Shirika la Mzinga kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na TAWIRI lilitekeza maagizo hayo na kufanikisha kutengeneza bomu baridi kukabiliana na tembo hao.
Katika hotuba yake ya uzinduzi wa bomu baridi la kukabiliana na tembo, Waziri Tax amelishukuru Shirika la Mzinga kwa kutengeneza bomu hilo baridi na akalitaka Shirika la Mzinga kuendelea kufanya utafiti wa kuliboresha bomu hilo kadiri inavyotakiwa ili liweze kuleta matokeo tarajiwa. Aidha, Waziri wa Ulinzi akasema ili bomu hilo liwe na matokeo chanya ipo haja ya kuzingatia na kufuata mwongozo wa matumizi uliotolewa na mzalishaji wa bomu hilo, kuzingatia utaratibu wa kuyahifadhi na kuyatunza mabomu haya na kuzingatia matumizi bora yaliyokusudiwa.
Waziri Tax akatoa wito kwa Shirika la Mzinga kuliboresha bomu hilo kwa teknolojia rafiki ili kuepusha madhara katika matumizi na kuliagiza Shirika la Mzinga na TAWIRI kuendelea na utafiti zaidi ili kuliongezea ufanisi katika utendaji.
Vile vile Waziri wa Ulinzi na JKT amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuliwezesha Jeshi kupitia Mashirika yake kwa rasilimali fedha, Vifaa na Wataalamu hivyo kulifanya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutekeleza majukumu yake kwa weledi.
Awali akitoa taarifa kwa Mhe. Waziri wa Ulinzi, Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga Brigedia Jenerali Seif Hamis amesema kuwa bomu lililofanyiwa utafiti na kutengenezwa na Shirika hilo liko katika aina mbili ambapo wabunifu bomu linaloweza kulipuka likiwa angani na lingine linaloweza kulipuka baada ya kutua ardhini. Pia, Brigedia Jenerali Hamis ameongeza kuwa Shirika la Mzinga kwa kushirikina na wadau wengine kama Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori litaendelea na tafiti mbalimbali ili kuwezesha kutokomezwa kwa tatizo la tembo kuvamia makazi ya watu.
Naye Naibu wa Maliasili na Utalii Dustan Kitandula ameishukuru Wizara ya Ulinzi na JKT kupitia Shirika la Mzinga kwa ubunifu wa bomu baridi litakaloleta tija katika kutatua changamoto za tembo kwenye makazi ya watu.