Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,070
- 716
WAZIRI WA ULINZI NA JKT AMKABIDHI GARI MOJA JENERALI CHELESTINO MSOLA (MSTAAFU)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 30 Aprili, 2024 amemkabidhi Meja Jenerali Chelestino Elias Msola (Mstaafu), gari jipya la kisasa ikiwa ni kutambua na kuthamini mchango wa utumishi wake kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Taifa kwa Ujumla.
Waziri Tax amempongeza Jenerali Msola (Mstaafu) kwa Utumishi wake wa uadilifu na uaminifu na kustaafu kwa heshima na akamtakia kila la kheri katika maisha mapya ya kustaafu.
Waziri wa Ulinzi na JKT amemshukuru Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Wanajeshi katika Ulinzi na maendeleo ya Taifa.
Aidha, Waziri Tax alimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT kwa kuhakikisha magari ya Wastaafu yananunuliwa kwa wakati.
Hafla hiyo ya kumkabidhi gari Jenerali mstaafu Msola, ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe.