Waziri wa Ulinzi na JKT afanya ziara ya kikazi kikosi cha 834 Makutupora

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,051
687
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax (Mb), leo tarehe Aprili 18, 2024 amefanya ziara ya kikazi katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya 834 Makutupora iliyopo Makutupora jijini Dodoma. Mhe Dkt Stergomena L. Tax, ni miongoni wa viongozi waliopata mafunzo ya JKT katika kambi hiyo mwaka 1983, katika Oparesheni Mshikamano.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la Kufuatilia na kujionea hali ya mafunzo ya vijana na jinsi Jeshi la Kujenga Taifa linavyotekeleza majukumu yake ya msingi ya malezi ya vijana, uzalishaji mali na jukumu la Ulinzi wa Taifa.
Katika ziara hiyo, Waziri Tax alilipongeza Jeshi la Kujenga Taifa kwa jinsi linavyotekeleza majukumu yake kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa, malezi na mafunzo kwa Vijana, katika shughuli za uzalishaji mali, na ushiriki wake katika Miradi ya Kimkakati ikiwa ni pamoja na Ulinzi na Uangalizi wa Bonde la Mzakwe unaofanywa na Kikosi cha 834 Makutupora.

Awali, akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na JKT, Kamanda Kikosi 834 kikosi cha Jeshi, Luteni Kanali Petro Mbanga, alimfahamisha Waziri wa Ulinzi kuwa kikosi hicho kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya mafunzo na malezi kwa vijana, uzalishaji mali na ulinzi wa Taifa kwa ufanisi, na akamfahamisha Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na JKT utayari wa kikosi hicho katika kushiriki shughuli zote na majukumu kitakachopangiwa na Serikali
Waziri Stergomena Tax katika ziara yake hiyo ya kikazi 834, alitembelea na kukagua sehemu za kulala vijana wa kike waliopo kikosini hapo kwa kujitolea na kwa mujibu wa Sheria.

Aidha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alitembelea shughuli za Uzalishaji mali katika kiwanda cha vifungashio kilichopo kikosini hapo, kilimo cha mbogamboga katika green house, ufugaji wa kuku na mayai na nyama. Waziri wa Ulinzi na JKT alielezwa na Kamanda Kikosi jinsi vijana wanaofanya mafunzo wamekuwa wakinufaika kwa kupata mafunzo ya stadi za kazi kwa vitendo kupitia na miradi hiyo.

Waziri Stergomena Tax aliongoza shughuli za Upandaji miti kikosini hapo kama sehemu ya kuhamasisha utekelezaji wa agizo la Serikali katika utunzaji wa mazingira.

Katika ziara hiyo ya kikazi 834 KJ Waziri Tax alisisitiza umuhimu wa kuwaanda vijana waliopo kwenye mafunzo. Akiongea na vijana wanaoendelea na mafunzo, aliwaasa kuitumia nafasi hiyo waliyoipata kuhudhuria mafunzo hayo kwa kuzingatia mafunzo wanayopatiwa na hatimaye wawe raia wema, wazalendo, walinzi wa Taifa, na kuweza kujiendeleza kiuchumi na kujitegemea pindi wamalizapo mafunzo.

 
sema i don't like kabisa kazi ya jeshi kuwa ni kufuga kuku na kulima.. JKT ilipaswa kuna one stop of finest engineers and scientists.

Israel kila askari ni meja au ni afisa kwa sababu kwenda jeshini ni lazima na wanaenda waliopita vyuoni, na vijana waliopigana gaza wamepata offer ya kulipiwa gharama za degree na masters
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…