Waziri wa Mambo ya Nje, Mahmoud Thabit Kombo awasili Finland kwa ziara ya kikazi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,022
678
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amewasili nchini Finland kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 08 hadi 11 Oktoba 2024.

Alipowasili kwenye Uwanja wa ndege jijini Helsink, Mhe. Waziri Kombo alipokewa na Balozi wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Theresa Zitting na Balozi wa Tanzania nchini Finland mwenye makazi yake Stockholm, Sweden, Mhe. Grace Ulotu.

20241009_073653.jpg

Katika ziara yake hiyo, Mhe. Waziri Kombo pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland, Mhe. Elina Valtonen Oktoba 09, 2024.

Aidha, Mhe. Kombo na Mwenyeji wake watashiriki kikao cha pili cha mashauriano ya kisiasa (political consultations) kama wenyeviti wenza wa mashauriano hayo. Kikao hicho kitajadili masuala mbalimbali ya ushirikiano yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili.

20241009_073654.jpg

Vile vile, Mhe. Kombo na ujumbe wake watashiriki mikutano ya kibiashara inayolenga kuvutia kampuni kubwa za nchini Finland kuja kuwekeza Tanzania katika maeneo mbalimbali kama vile Misitu, Nishati, Tehama, Utalii na Elimu.
20241009_073657.jpg

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Kombo ameambatana na viongozi waandamizi wa Serikali kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TANTRADE).
 
Attachments

  • 20241009_073650.jpg
    20241009_073650.jpg
    495.4 KB · Views: 1

💪speed and standard,
well done ndugu waziri Kombo 🌹
 
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Kombo ameambatana na viongozi waandamizi wa Serikali kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na Mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TANTRADE
Waziri wetu amekaa kama vile hajiamini na anachokifanya
 
Katika mawaziri ambao wananchi hawawajui ni huyu, nadhani ofisi yake au serikali imuandalie tukio la kumtambulisha nchini kwetu, afanye hata media tour. Anayoyafanya ni kwa ajili yetu, alete retirement. Hivi ni mtoto wa Mh. Thabiti Kombo?
 
Back
Top Bottom