Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako alikosea kuivunja Bodi ya TCU

KAPONGO

JF-Expert Member
May 29, 2009
1,682
676
Uamuzi wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako wa kuwasimamisha kazi viongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania -TCU kwa maelezo kuwa pamoja na mambo mengine iliwadahili wanafunzi wasiokuwa na vigezo, sasa unaakisi taswira ambayo inaaminisha kuwa uamuzi ule ulikuwa wa kukurupuka, usio na tija na uliokiuka taratibu za kiutawala.

Hiyo inatokana na kuibuka wiki hii kwa taarifa kutoka ndani ta TCU ikielezea kuwa kumbe serikali yenyewe (ya awamu ya nne) ndiyo iliyobuni mwaka 2013 mpango maalum wa kudahili wanafunzi wa kidato cha nne waliofaulu masomo ya sayansi ili waandaliwe mafunzo maalum ya stashahada ya ualimu wa masomo ya sekondari. Lengo likiwa ni kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi nchini.

Kama hivyo ndivyo ilivyo Waziri Ndalichako hakuwa na sababu ya kukurupuka kuwasimamisha wajumbe wa bodi hiyo kwa kosa ambalo serikali yenyewe ndiyo iliyoasisi. Na ni kosa kubwa Zaidi kuwafukuza na kuwatelekeza wanachuo 7,000 walikuwa wakiendelea na masomo yao Chuo kikuu Dodoma na mahali kwengine, kwa makosa yaliyofanywa na serikali yenyewe.

Matukio kama haya hayana budi kuangaliwa kwa jicho pevu ili kudhibiti kuwaumiza raia wasio na hatia, na kulinda na kudumisha utawala wa haki na kisheria. Waziri angepaswa kujiridhisha na kujitosheleza kwa hoja na mantiki kuhusu ubaya na uzuri wa falsafa ya serikali ya awamu iliyopita ya kutaka kuziba pengo la upungufu wa walimu wa sayansi kwa mtindo huo wa 'voda fasta' ili kuondoa mapungufu hayo ili lengo la msingi lifikiwe, kwani hakuna ubishi kuwa kuna upungufu mkubwa wa walimu nchini katika ngazi zote za elimu! na kwamba wahitimu wa vyuo vikuu wanaofaulu vizuri ualimu si fani yenye mvuto kwao kutokana na serikali kutowalipa vizuri,ukilinganisha na fani nyingine.

Na hapo umuhimu wa kuwa na dira ya taifa ya Muda mrefu ndipo unapojitokeza!
Na kwa vile kujikwaa si kuanguka, ni matarajio yangu kuwa Prof atatambua alikopotoka au kupotoshwa na atachukua hatua maridhawa kurekebisha kasoro hiyo, hususan kuwarejesha masomoni wanachuo wale waliopoteza muda na fedha zao kusomea kozi iliyobuniwa na serikali, na baadaye serikali hiyo hiyo ikaisitisha!
Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi waliotimuliwa Ni wale wa diploma maalumu...........
 
Suala la UDOM ni kugoma kwa wahadhiri na suala la TCU ni kudahili wanafunzi ambao hawana sifa usichanganye mafile.

unajua sababu za kugoma kwa wahadhiri??
ni kwamba serikali iliacha kuwalipa ujira wa kufundisha diploma so fununu za kuwatoa wanafunzi wa dip toka mwezi wa 3 but chuo kikawa na mgogoro na ndalichako kipitia nacte so amri ya kuwasimamisha masomo ilitoka kwa mtumbua majipu

au kwa lugha rahisi tunaweza sema hii program ya special diploma udom ilikua inapewa mkono na wamarekani kupitia MCC sasa MCC walijitoa kufadhili sasa unategemea nn???
 
au kwa lugha rahisi tunaweza sema hii program ya special diploma udom ilikua inapewa mkono na wamarekani kupitia MCC sasa MCC walijitoa kufadhili sasa unategemea nn??? aaa
 
mama ndali aangalie kwa umakini...hao watumishi wanaosema hawana vigezo ndio hao walikuwemo miaka nenda rudi...si vizuri kuwafukuza kama mbwa!
 
Kichwa maji unachanganya mambo! Swala la UDOM ni mgomo wa wahadhiri!

Swala la kusimamishwa vigogo wa TCU ni kutokana na kudahiri wanafunzi wasio na sifa!

Haya ni maswala mawili tofauti ...
 
naona umechanganya mafaili mkuu
 
Hili ni tatizo la muda mrefu la sisi wabongo. Kabla mtu hajajua vizuri anataka kuandika nini anakurupuka kukosoa. Kumbe yeye ndiye wa kukosolewa.
 
dah .. hii awamu ya jpm ni janga sasa. Ndalichako ajiuzulu tu, hana namna kwa kweli.
 
Hata kama ni mpango maalum wataalamu wetu njaa inapasa wawe na uwezo wa kuiambia serkali "hili hapana"lkn,sababu wanasubiri zawadi ya udc wanaacha taaluma zao na kuwa mabwana ndo.
 
Nilimsikia Waziri akisema kwamba TCU imewadahili wanafunzi ambao hata hawana sifa za kushiriki kwenye kozi ya ngazi ya diploma. Kama ilikuwepo program ya kupata walimu kwa mtindo huo mimi naona haingewezekana. Hata upe iliua elimu hivyo hivyo kuwachukua darasa la saba waliofeli kisha wakafundishe darasa la saba unategemea nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…