Waziri Ulega Atoa Maelekezo Ujenzi wa Barabara ya Mbande - Msongola (3.8 KM) Ukamilike kwa Wakati na Ubora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,717
1,246

WAZIRI ULEGA ATOA MAELEKEZO UJENZI WA BARABARA YA MBANDE -MSONGOLA (3.8 KM), UKAMILIKE KWA WAKATI NA UBORA.

Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega, leo Jumamosi tarehe 28 Desemba 2024, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mbande hadi Msongola yenye urefu wa kilometa 3.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Akiwa kwenye ziara hiyo, Waziri Ulega amesisitiza uharaka, kasi na ubora wa utekelezaji mradi huo huku akitoa maelekezo mahususi kwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na mkandarasi wa mradi, kampuni ya Jonec (T) Limited.

Akizungumza na wananchi wa Msongola, Waziri Ulega amesisitiza kuwa mkandarasi ahakikishe kazi inafanyika usiku na mchana, kuongeza wafanyakazi na vifaa, na kukamilisha ujenzi kabla ya mvua za masika.

"Wananchi wanataka kuona thamani ya fedha zao. Haiwezekani barabara ijengwe chini ya mwaka mmoja kisha iharibike. Ukijenga chini ya kiwango, utarudia kazi kwa gharama zako mwenyewe." alisema Waziri Ulega

Ziara hiyo pia iliibua ombi la wananchi la kuwekwa taa za barabarani katika eneo la Msongola Center ili kuwezesha shughuli za biashara hadi usiku na kupunguza uhalifu.

"Nataka kuona Msongola inang'aa kwa taa za barabarani, na wananchi waendelee kufanya biashara zao kwa amani na usalama hata nyakati za usiku," aliongeza Waziri Ulega.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema barabara ya Mbande-Msongola ni muhimu kwa kuunganisha wilaya za Ilala, Temeke, na Mkuranga, huku akisisitiza usimamizi wa karibu kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi John Mkumbo, amebainisha kuwa ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 50.5, na mkandarasi tayari amelipwa fedha zote.

Mbunge wa Ukonga, Mheshimiwa Jerry Silaa, ametoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuhakikisha barabara hiyo inajengwa kwa urefu wa kilometa 3.8 kwa mara moja, tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilijengwa kilometa moja kwa mwaka.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.09.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.09.jpeg
    564.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.10.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.10.jpeg
    467.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.11.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.11.jpeg
    510.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.11 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.11 (1).jpeg
    439.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.10.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.10.jpeg
    467.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.14.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.14.jpeg
    122.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.14 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.14 (1).jpeg
    133.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.13.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.13.jpeg
    537 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.12.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-28 at 21.37.12.jpeg
    430.6 KB · Views: 3
Barabara ikamilike watu wapitie miez kadhaa nilienda ilikua bado had leo bado halafu ni km3 tu. Sema hili jimbo ni kubwa sana limemvaa Jerry
 
Hongera Mh Waziri na Mbunge Jerry.
Hivi Mbunge wa Kibamba yupo kweli, barabara za huku ni mbovu na mvua hizi.
Mh Waziri karibu Kibamba barabara ya Mbezi lous(Victoria) - Mpigi Magohe -Bunju na barabara zote za Mbezi na Kibamba.
 
Mnawalipa Wakandarasi lakini? sio kuhitaji barabara zikamilike huku wakandarasi hawapati malipo yao!
 
Yaani hiyo barabara itakayounganisha Nyerere road na Kilwa road ndio itakayobadilisha hadhi ya Kivule na Kitunda kama ambavyo barabara ya Goba iliyounganisha Morogoro road na Bagamoyo road.
 
Back
Top Bottom