Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,418
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo amesema hakuna kanuni/sheria inayompa mamlaka RC kumchapa mwanafunzi yoyote yule viboko kwani mwongozo wa uendeshaji wa elimu umetoa utaratibu wa adhabu kwa wanafunzi. Jafo amesema bado anasubiri taarifa ya RC wa Mbeya kuhusu tukio hilo.
Rais Magufuli
Nilikuwa nazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, nikamwambia ulitakiwa uwatandike viboko kwelikweli na uwafukuze shule, na natangaza hapa kuwa wale wanafunzi wote wamefukuzwa Shule na bodi ile imevunjwa kwasababu ni uzembe wa bodi mpaka mambo yale yametokea.
Nampongeza RC Mbeya, ila kwa wale watoto waliotimuliwa shuleni lazima wazazi wao walipe, nasema haya sio kwa sababu sina huruma nimeshawahi kuwa mwalimu, nawaomba wazazi nafikiri kuna mahali tumekosea ni sheria kuhusu viboko.
Je, tumfuate nani?
1. Wateule?
2. Rais?
3. Katiba/Sheria?