Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,591
- 1,191
Waziri Tabia Mwita Afungua Kongamano la Saba la Kiswahili la Kimataifa (Kiswahili na Diplomasia Duniani)
Serikali ya Zanzibar imesema lugha ya kiswahili ina mchango mkubwa katika kukuza diplomasia ya uchumi hivyo ni wajibu kwa taasisi zinazofundisha lugha hiyo kuongeza kasi ya kuikuza na kuieneza duniani.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia M. Mwita alisema hayo alipokuwa akifungua kongamano la saba la Kiswahili la Kimataifa hafla ambayo imefanyika katika ukumbi wa Shekh Idrisa Abdulwakili Kikwajuni.
Alisema katika kukabiliana na hatua hiyo ni jambo la msingi kuongeza program za ufundishaji kwa walimu wa ndani na nje ili kuifundisha lugha hiyo katika maeneo mbalimbali.
Sambamba na hayo Waziri Tabia alisema dipromasia ya lugha ya kiswahili ni lugha rasmi ya muungano wa Afrika inayosaidia kusukuma mbele na ajenda ya Afrika Mashariki ambayo ni moja ya kipaumbele cha uchumi wa Afrika na duniani kote.
Alisema katika kuthamini lugha hiyo hivisasa katika vyuo vikuu na vyuo vya uwalimu kunamwamko mkubwa wa wanafunzi kuisoma lugha hiyo kutokana na kupewa kipaumbele kikubwa duniani.
Mbali na hayo Tabia alitumia fursa hiyo kuwataka washiriki wa kongamano hilo kulitumia ipasavyo ili liwekichocheo cha bidhaa bora zinazosambaza matumizi ya kiswahili fasaha na sanifu katika shughuli mbalimbali.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab alisema lugha ya kiswahili hivisasa imekuwa kutokana na baadhi ya wageni kununua makamusi ya kiswahili na kwenda kufundisha ndani ya nchi zao.
Alisema hatua hiyo imesaidia kukifanya kiswahili kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwa mustakabali mwema wa nchi na taifa kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili, Dk Saade Said Mbarouk alisema baraza linaendelea kutoa mafunzo kwa walimu wa lugha ya kiswahili ili kuwafundisha wageni kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kueneza lugha hiyo duniani.
Alisema kiswahili hivisasa kimekuwa zaidi ya lugha nyengine kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na BAKIZA katika kuitangaza lugha hiyo duniani.
Kongamano hilo la saba lenyekaulimbiu" Kiswahili ni zaidi ya lugha tuitumie kuimarisha Diplomasia