Waziri Simbachawene aonya Wakuu wa Taasisi za Umma: Aliyekwambia unafaa nani?, Cheo ulipata kwa chapuo, tukikuchunguza unakuta ndio wezi na wapigaji

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
2,322
6,378
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, ameonya vikali wakuu wa taasisi za umma dhidi ya upendeleo na mianya ya rushwa katika teuzi zao.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Simbachawene alieleza kuwa baadhi ya viongozi wanawateua watu kwa majina badala ya kuzingatia sifa na uwezo wao. "Cheo ulipata kwa chapuo, halafu na wewe unaleta watu kwa majina. Aliyekwambia unafaa nani?" alihoji kwa ukali.

"Tukikuchunguza tunakuta ndio wale wezi, wapigaji na wala rushwa." alisisitiza.

Mambo mengi kwenye nchi hii yanafeli Kwa sababu ya viongozi wetu Wana uwezo mdogo sana wa kufanya maamuzi.

Viongozi wanapatikana Kwa rushwa na upendeleo wa kindugu, sasa hapo ufanisi utatoka wapi !?
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, ameonya vikali wakuu wa taasisi za umma dhidi ya upendeleo na mianya ya rushwa katika teuzi zao.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Simbachawene alieleza kuwa baadhi ya viongozi wanawateua watu kwa majina badala ya kuzingatia sifa na uwezo wao. "Cheo ulipata kwa chapuo, halafu na wewe unaleta watu kwa majina. Aliyekwambia unafaa nani?" alihoji kwa ukali.

"Tukikuchunguza tunakuta ndio wale wezi, wapigaji na wala rushwa." alisisitiza.

Yeye mwenyewe ni mwizi balaa.
 
Back
Top Bottom