Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,886
- 13,641
Kusema kweli CHAPUTA nayo isisajiriwe kama Taasisi ya Kijamii.Hizi shule mwisho wa siku zitakosa wanafunzi.
Watu hawataki kuzaa maisha magumu
Jina lake la ukoo ni Silaa/Silaha/Si-raha/Slyaa/Slaa au linaandikwaje?Hebu ukiwa unachukua taarifa mpe kalamu aandike linavyotamkwa.Kubadili uandishi halali wa jina la mtu ni kosa.Waziri Habari, Mawasiliano na Teknilojia ya Habari, Jerry William Silaa ameweka jiwe la msingi Shule Mpya ya Sekondari Sekoutoure iloyopo Kata ya Ilongero Wilaya ya Singida kuashiria uzinduzi rasmi wa shule hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni moja.
Shule hiyo mpya iliyojengwa ililenga kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule ya sekondari Ilongero na kuwapunguzia adha wanafunzi kutembea umbali mrefu baadhi ya wanafunzi waliokua wakisoma shule ya Sekondari Ilongero imezinduliwa rasmi leo Oktoba 25, 2024.
Akizungumza maara baada ya kukagua majengo na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo Waziri Silaa amesema hiyo ni sehemu tu ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu nchi nzima ikiwa ni pamoja na Mkoa wa singida.
Ametoa rai kwa wanafunzi wa shule hiyo mpya iliyoanza rasmi januari 2023 ikiwa na idadi ya wanafunzi 483 hadi sasa kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa kuwa tayari Serikali imeweka miundombinu bora katika shule hiyo.
Akitoa taarifa ya Mradi wa shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Sekoutoure Tatu Njaku amesema ujenzi wa shule hiyo umeboresha mazingira ya Kufundishia na wanafunzi kujifunza.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego kwa ujumla wake amesema kwa kipindi cha miaka Mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Singida unashule mpya za sekondari 33 ikiwa ni kuendelea kupunguza changamoto za wanafunzi kusoma umbali mrefu.
Waboreshe mazingira kwa kupanda nyasi (ukoka) ndani ya maeneo yote yaliyozungushwa mawe, itapendeza zaidi na muonekano wa uzuri utadumu.Shule nzuri sana hii
Hilo ni kweli mkuuWaboreshe mazingira kwa kupanda nyasi (ukoka) ndani ya maeneo yote yaliyozungushwa mawe, itapendeza zaidi na muonekano wa uzuri utadumu.
Kwa idadi ya hayo Majengo (14) ukifanya makadirio ya shilingi milioni 50 Kwa Kila Jengo, unakuta gharama halisi ni kama milioni 700 hivi
Sasa hiyo bilioni 1 imetoka wapi au ndiyo kula Kwa urefu wa kamba??π
Nimekupata bossKiongozi unaweza kuwa sawa kabisa japo ujue shule sio majengo pekee;
1. Yaweza kuwa kwenye hayo majengo kuna maabara ya kueleweka inayo gharimu fedha nyingi
2. Madawati ya chuma ya kueleweka
3. Computer Lab ya kueleweka
5. Na kwa sababu ni mpya kuna vitabu vingi na vifaa kadhaa vimenunuliwa + Library
6. Ingefaa, ningependekeza wajiri na mwalimu wa Hesabu/Physics & Biology kabisa kwani hao ni hadimu
Mkuu kuna hadi nyumba ya vyumba vitatu inayo gharimu M15 na nyingine ya vyumba vitatu inayo gharimu M100!!Nimekupata boss
Naungana na Wewe MkuuMkuu kuna hadi nyumba ya vyumba vitatu inayo gharimu M15 na nyingine ya vyumba vitatu inayo gharimu M100!!