Waziri Prof. Mkenda apiga Marufuku wanafunzi waliopata Matokeo mabaya kufukuzwa shuleni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,688
1,240
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amepiga marufuku kwa baadhi ya shule ambazo zimekuwa zikiwafukuza wanafunzi baada ya kuwa na matokeo mabaya katika matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili

Waziri Mkenda amepiga marufuku hiyo, Jumanne Januari 9.2024 Jijini Dodoma baada ya kutembelea Shule ya mfano ya Sekondari iliyopo kata ya Iyumbu ili kujionea maendeleo ya ujenzi

“Kama kweli Shule ni bora inatakiwa ihakikishe inamfundisha vizuri mwanafunzi na afaulu sio akifeli mnamfukuza wakati mmeshachukua ada za Wazazi hili jambo sio sawa waleeni Watoto mpaka wamalize masomo yao vizuri" -Prof. Mkenda

Pia, Prof. Mkenda amepiga marufuku kwa shule za serikali kuweka michango ya lazima ambayo mzazi asipoitoa mtoto hawezi kwenda shule

Amesema, baadhi ya shule zimekuwa zikiweka michango ambayo inapelekea mtoto kushindwa kwenda shule ikiwa serikali imesema elimu inatolewa bure

Mbali na hayo Prof. Mkenda amezungumzia Sekondari ya mfano iliyopo Kata ya Iyumbu, Jijini Dodoma ambayo ina wanafunzi 138 ambapo amesema imejengwa kwa ajili ya mchepuo wa sayansi lakini kwa sasa imeanza kwa michepuo ya masomo ya sanaa kutokana na maabara kutokukamilika kwa wakati

Amesema kuwa Shule hiyo inatarajiwa pia kuwa na mkondo wa mafunzo ya amali ili wanafunzi wasome mafunzo ya ufundi kwa vitendo ikiwemo masomo ya uhandisi na mengineyo ya Sayansi

"Kwa sasa Shule hii haina jina rasmi na kuna mapendekezo yametolewa ila siku ya uzinduzi tutalitangaza jina rasmi la shule hii ambayo kwa sasa imeanza kuchukua wanafunzi wa mkondo wa masomo ya sanaa na sababu kubwa ni kutokana na kutokukamilika Kwa maabara kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa masomo ya sayansi" -Prof. Mkenda

Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Devis Mwamfupe amesema kuwa shule hiyo ni jitihada za dhati za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutaka watoto wa kitanzania kupata elimu bora na katika mazingira bora na kumshukuru Kwa kuchagua Dodoma kujengwa shule hiyo ya mfano

"Serikali ya awamu ya sita chini Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha elimu inatolewa kwa viwango vikubwa, ndio maana shule za siku hizi zinajengwa kisasa na shule hii ya mfano hapa Iyumbu ni moja ya shule bora," -Prof. Mwamfupe

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT Kanali Peter Ngata amesema mradi huo wa ujenzi wa shule hiyo imefikia asilimia 96 kukamilika huku akimhakikishia Waziri wa elimu kuwa shule hiyo itakamilika kwa asilimia 100 ndani ya mwezi mmoja kutoka sasa.

GDeefmiW0AA1SLI.jpg
GDeef1CWgAA5yFo.jpg
GDeegD2WIAAMm58.jpg
 

Ni kama vile viongozi waliwekwa kikao wakaambiwa kila wanapoongea wahakikishe wanalitaja jina la Rais.
 
Back
Top Bottom