Kusoma sakata lilipoanzia soma hapa
- Sakata ujenzi wa Shule kwenye uwanja mpira Panga - Tegeta Wazo kuna harafu ya Rushwa na uzembe, tunaomba TAKUKURU ilimulike
- Waziri Ndumbaro Asitisha Ujenzi wa Shule Eneo la Michezo Dar
Kufuatia malalamiko hayo mdau kupitia andiko lake ambalo alileta jukwaani alieleza zoezi hilo halikuwa shirikishi kwa Wananchi ambao ndio walikuwa wanufaika na watumiaji wa uwanja.
Waziri alifika eneo hilo na kukutana na Wananchi na kudai suala hilo lilikuwa likifanyika kinyume, ambapo alieleza kuwa aliangizwa na Rais kwenda eneo hilo, akatoa Saa 72 wahusika waliokuwa wanachimba msingi (waliodai kuwa ni Shule) kusitisha zoezi na kusawazisha eneo hilo na kuuweka uwanja katika hali ya kawaida kama ilivyokuwa awali.
Sisi Wananchi wa eneo hilo, tunaona linazidi kuharibika hasa wakati huu ambapo mvua zimekuwa zikinyesha mara mojamoja.
Nini kinaendelea nyuma ya pazia, je, maelekezo ya Waziri yamepuuzwa? Wananchi tulipata matumaini kwamba kilio chetu kimesikika na Waziri alitueleza mipango kabambe kuhusu uendelezwaji wa uwanja huo kwamba wanapanga kuuendeleza, lakini tunashangaa hali ipo vile vile hawajasawazisha chochote wala ujenzi haurndelei lakini vifaa vya ujenzi bado vipo saiti.
Aliyeandika awali kabisa hapa JF alitoa wito kwa mamlaka za juu ikiwemo TAKUKURU kumulika suala hilo akidai kuna viashiria vya uwepo wa Rushwa na ukiukwaji wa Sheria.
Nikazie hapo, tunaomba mamlaka zitueleze nini kinaendelea eneo hilo ambacho kinapelekea maelekezo ya Waziri kushindwa kutekelezwa. Lakini pia tunajiuliza imekuwaje Waziri ameshindwa kufuatilia utekelezwaji wa maelekezo yake au kauli yake ilikuwa kiini macho ili kutupunguzia hofu sisi wananchi.