OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Waziri wa Mawasiliano, Nape Nnauye akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Mkoa ya Rufaa, Lindi amejisifu kuwa na digital divide kubwa mbali na kuwa yeye ndiye Waziri wa mawasiliano, tukiamini anafanya kazi kuhakikisha watu wanakuwa online kama ambavyo bajeti ya serikali ya mwaka 2023/24 na Rais Samia wamejinasibisha kutaka watu wote wawe connected.
Nape amesema walioko mtandaoni ni 16% ambapo 40% kati yao wako nje ya nchi. 40% ya 16% ni 6.4%. Maana yake ni kwamba watanzania walioko Tanzania ambao wako mtandaoni ni 9.6%.
Wakati huo TCRA wanatuonesha kwamba kwa mwezi Juni 2023 kulikuwa na digital devices 34,047,407 zilizokuwa subscribed mtandaoni. Devices hizi zinaonesha kwamba watu wengi wapo connected tofauti na anavyosema Waziri, je nani tumuamini?
Tuendelee. Kwa kuwa watanzania 9.6% ya watanzania ndio wako mtandaoni maana yake katika vifaa milioni 34 vinavyotangazwa na TCRA ni vifaa 3,273,837 ambavyo vina access ya mtanadao.
Hata hivyo kwa watanzania milioni 61, tukisema waliokuwa connected ni 9.6% maana yake ni watanzania 5,856,000 walioko mtandaoni.
Rais Samia aliwahi kusema kwamba anataka kuona watanzania 100% wanakuwa mtandaoni kufikia mwaka 2030. Bajeti ya serikali na sera ya TEHAMA zinaonesha nia ya kutaka watanzania kuwa connected lakini Waziri anayesimamia suala hilo anajisifu Watanzania wachache kuwa mtandaoni. Je, Tanzania ya kidigitali itafikiwa?