Waziri Nape, kuhusu vifurushi vya simu tatizo lipo TCRA

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
92
1,685
NDUGU NAPE, KUHUSU VIFURUSHI VYA SIMU

Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.

Ndugu yangu Nape tatizo liko hapo TCRA. Haya makampuni ya simu yanafanya biashara na hivyo yanaweza fanya lolote yasipopata usimamizi.

Tunahitaji Kanuni za vifurushi kama vifurushi kutoka hapo TCRA ili zitusaidie

Kanuni iliyopo haitambui Vifurushi. Hakuna popote katika Kanuni yote ya Gharama za Simu THE ELECTRONIC & POSTAL COMMUNICATIONS (tarrifs) REGULATION 2018 linapotajwa neno Kifurushi/Bundle.

Hii maana yake makampuni ya simu hayachukulii Kifurushi kama mawasiliano rasmi bali yanaita vifurushi OFA/MSAADA

Mawasiliano yote ya Maandishi (ambayo ninayo) na ya Mazungumzo(vikao) niliyofanya na makampumi ya simu wanaita Vifurushi OFA.

Yaani eti, zile pesa zote tunazotoa kujiunga kwenye internet, mazungumzo, na SMS wanakuwa wametupa OFA (msaada). Usipokuwa mvumilivu unaweza kumtia mtu ngumi.

Wanasema eti mda wa mawasiliano rasmi ni ule unaotumia pesa/salio la kawaida la kwenye simu bila kujiunga. Ukijiunga Kifurushi hiyo ni kitu kingine, ni Ofa.

Kinachosikitisha zaidi, TCRA nao wanakubaliana na hili jambo kuwa kifurushi ni Ofa/msaada. TCRA wameniambia mimi hivyo ktk vikao nilivyofanya nao kuhusu hili jambo na barua zao ninazo wamenijib wakisema hivyo hivyo.

Kwa msingi huu wa Bando kuwa Ofa (msaada) maana yake ni kuwa anayetoa Ofa ndiye pia hutoa masharti ya Ofa. Ikiwa utapewa Ofa ya Lunch basi huna uwezo wa kumwambia aliyekupa Ofa kuwa lazima na supu ya kuku iwepo.

Vivyo hivyo ndivyo wasemavyo watoa Ofa(msaada) ya vifurushi kuwa wewe mnunuzi wa Kifurushi mpewa Ofa(Msaada) huwezi kuweka masharti kuwa kifurushi chako kisiexpire, bali wao ndio wanaamua hiyo Ofa(msaada) itumikeje.

Kwahiyo Ndugu zangu lile suala letu tunalokataa siku zote kuwa huwezi kuniuzia kifurushi nikakulipa hela zako zote, halafu ukanizunguka ukakichukua tena kwa mwavuli wa muda wake kuisha linakwama hapa.

Sasa ndugu Nape atusaidie. Tuwe na Kanuni inayotambua vifurushi kama ilivyo kwa Salio la kawaida(Tariff). Na tabia ya kuita kifurushi tunachonunua kwa jasho letu Ofa, ikome.

Kanuni iratibu vifurushi kama vifurushi, iviwekee ulinganifu wa matumizi(rates), uwezo wa kuhamishiana, iondoe muda wa kuexpire, itambue kifurushi kama mali ya mnunuzi, iweke mfumo mzuri wa mtumiaji mwenyewe kuweza kufuatilia matumizi ya kifurushi chake, na mengine mengi mazuri.

Kwanini kifurushi kihitaji kanuni zake zinazojitegemea ??. Ni kwasabab hakuna shaka kuwa Kifurushi ndio mawasiliano sasa hivi.

Zaidi ya 90% ya watumiaji wanatumia vifurushi. Wanaotumia Salio la kawaida bila kujiunga ni kama hawapo kabisa kwasasa.

Sasa unawezaje kuwa na Kanuni ya kuratibu Matumizi ya Salio la kawaida ambayo ndiyo tunayotumia, ukakosa Kanuni ya kuratibu Kifurushi ambacho ndicho matumiz haswaaa ya simu kwasasa.

Wakati mwingine tukiwashtaki makampuni ya simu kwa kukata vifurushi kwa kigezo cha kuexpire wamekuwa wakiuliza ni sheria gani waliyovunja.

Hakuna jibu kwakuwa hakuna sheria ya kuratibu vifurushi. Ndugu Nape atusaidie hili na liko ndani ya uwezo wake.

Kuhusu kesi yangu na Makampuni ya simu pamoja na harakati hizi za mawasiliano hasa vifurushi kwa ujumla vipo na vinaendelea, hii ni kwa wale ambao wamekuwa wakiuliza nimefikia wapi.
 
Mimi kwa upande wangu huwaa naaamin kuna vigogo wanahisa katka makampuni haya...ndo mana huwa hawana mda wa kuchek mambo kama haya
 
Umeeleza vizuri sana,ndio maana tunajiuliza hivi wale Wabunge kule bungeni wanamuwakilisha nani hasa?

NB:Kuhusu Kesi yako na makampuni umekuwa mzito wa kuleta mrejesho hasa ikizingatiwa kwamba wakati unaweka nia ya kuyashtaki makampuni ulileta Uzi humu.

Umesema inaendelea vizuri,je ni kwa namna ipi?
 
Mambo yalikuwa mazuri mpaka pale waziri mstaafu ndugulure alipoingilia mambo ya vifurushi
 
Back
Top Bottom