Waziri Mwigulu chukua hatua

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,372
8,469
Idara Ya uhamiaji imetangaza kusudio lake la kumshitaki bw. Yussuph Manji kwa makosa ya wafanyakazi wa kampuni za quality group kukutwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini yeye akiwa kama mmiliki wa kampuni

Lakini katika hali ya kushangaza idara hii ya uhamiaji imetangaza kumchukulia hatua Afisa uajiri wa kampun ya cement ya Dangote na si Mmiliki wa kampuni kama ilivyokuwa kwa Manji. Huku kunaitwa ni kujichanganya au kitaalam wanasema double Standard.

Hii inaakisi malalamiko ya siku nyingi dhidi ya jeshi la polisi kuwa watendaji wake wamekiwa na tabia ya kuwabambikia kesi watuhumiwa mbalimbali pindi wanapokuwa wamekosa ushahidi wa tuhuma zinazowakabili au hata kukiwa na ushahidi kuwapatia kesi nyingine zisizo zao

kwa mfano mtu anaweza kukamatwa kwa kesi ya wizi wa simu ukifika polisi utaambiwa pamoja na simu hii zimeibiwa laptop nne na tsh miillioni 2 hali wakijua si kweli au waweza tuhumiwa kwa kesi ya wizi ukapewa kesi ya mauaji pia kumekuwa na madai mengi ya kesi za kubaka za kupanga

Waziri Wa mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu bado tuna imani sana na wewe umepewa wizara nyeti mno Kwa usomi na ujana wako bado tunategemea makubwa toka kwako japo umeonyesha kufeli katika hatua za awali za cheo hiki

Ndg Mwigulu kama bado una ndoto za kugombea urais hii wizara ni nafasi yako ya kujiongezea point au kukuangusha hebu chukulia hili jambo la mihadarati ungelisimamia wewe (na ndivyo ilivyopasa) saa hizi ungekuwa na sifa nyingi mno. lakini bado una nafasi hujachelewa Simamia kulibadilisha jeshi la polisi haki inaanzia polisi lakini polisi wamekuwa ndio wavunjaji wakubwa wa haki hawasimamii haki hawatoi msaada wa kishweria kwa mtuhumiwa pindi inapohitajika wanachojua wao ni kumkandamiza mtuhumiwa kumdhalilisha na kumtesa kadri wawezavyo hata kama kosa lake haliitaji mateso polisi hawawezi kwepa lawama hizi

wito wangu kwako mh. mwigulu badilisha jeshi la polisi liwe chombo cha haki kwa raia
 
Tangu mwaka jana Manji alijitoa Quality Group...nimeshangaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…