Waziri Mwakyembe alionya wasanii kujihusisha na siasa

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,436
7,940
Kama waziri mwenye dhamana na wasanii, amewahi kutoa kauli kuwa haifai msanii kujihusisha na siasa na akaonya kuwa kama msanii anataka kujihusisha na siasa bora aache kazi hiyo ajiunge na siasa.

Alitoa hayo baada ya msanii Roma Mkatoliki kutekwa na kuachiwa na watu wasiojulikana.

Jana wasanii wakajazana kwenye uwanja wa Taifa kuimba nyimbo za kisiasa za CCM. Je, Mwakyembe ameshindwa kusimamia kauli yake?

Tanzania hatuna viongozi wanaosimamia kauli zao bali wasaka tonge, ndumilakuwili, wanafiki na wazandiki, wenye upendeleo wa wazi wazi.
 
Unataka wakatae kazi sasa watakula wapi?

Chadema walimchukua Msaga Sumu hata hela ya nauli hawampi mwaka huu kakimbilia sisiem.
 
Halafu tamasha lenyewe ni kama lilibuma, hao wasani walikuwa wanasema tu mara mikono juu, peleka kushoto kulia... sijui mara oyo oyo oyooo... watu kimya!

Kila mmoja anasema piga kelele kwa Magufuli, yaani ilikuwa ni vituko kwa kweli!

Mwisho wa siku wakaishia kuitana mabangi na kupigana mitama!!
 
Ndo hivyo mkuu kikubwa familia imepata chakula
Taifa la wanafiki siku zote halina maendeleo sustainable. Akija kiongozi mwingine mtamsapoti kwakusema aah yule aliyepita hiki hakufanya sahihi wakati mlimuunga mkono wakati wa utekelezaji wa hiko kitu.

Tujitathmini sana kama watanzania
 
Hatakiwi kujihusisha kwa upande wa upinzani na siyo tawala.

Kumbuka dunia haina usawa.
 
Back
Top Bottom