Waziri Muhongo amjia juu Zitto Kabwe, ni kuhusu kampuni ya IPTL

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,292
SIKU chache kupita baada ya Mbunge wa Kigoma mjini,Zitto Kabwe kusema tangu utawala wa Rais John Magufuli kuingia madarakani,Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imeitia hasara serikali ya Bilioni 36 kwa kile anachodai Kampuni hiyo inaitapeli serikali kwenye Malipo ya Capacty Charge,

Naye Waziri wa Nisharti na Madini,Sospeter Muhongo ameibuka na kusema Mbunge huyo anatumiwa kuisakama kampuni ya IPTL kwa maslahi yake kisiasa,

Waziri Muhongo ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam,wakati alipokuwa anazungumza na mwandishi wa Fullhabari.blogs mara baaada ya kumalizika mkutano na waandishi wa habari aliokuwa anazungumzia ugunduzi mpya wa Gesi asilia,

Ambapo Waziri Muhongo ni kama amemshangaa mbunge huyo kwa kitendo chake achodai ni kushikilia hoja ya IPTL kila siku badala ya kutamaza mikataba yote ya Makampuni ya umeme ambayo inauzia umeme Tanesco ambayo amekili ni mibovu,

“Yaani huyu mtu anaugomvi tu na hii kampuni na anaitumia kwa ajili ya kujijenga kisiasa,maana kila siku yeye na IPTL tu,kama hoja ni mikataba ni mbovu,ni makampuni yote yanayoiuzia shirika la umeme Tanesco mikataba mingi inakasoro nyingi,lakini nashangaa huyu Zitto ayasema haya kila siku na IPTL,mbona mengine hasemi”amesema Waziri Muhongo,

Waziri Muhongo ameongeza kuwa “na nyinyi wanahabri tumieni elimu yenu kuelimisha umma,tuache kuingia kwenye mitego ya wanasiasa wa aina hii,tusema ukweli juu ya mkataba wa IPTL na Tanesco”

Kauli ya Waziri Muhongo inakuja ikiwa Mbunge huyo ambaye ni Kiongozi wa mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo kuandika kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo aliandika kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia jumla ya bilioni 36 kupotea,

"Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Raisq, kwa kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe.

Aidha,Zitto Kabwe aliongeza kusema kuwa Wakati Rais Magufuli anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini,

"Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi.

"Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini.
 
Kumbe tatizo ni MIKATABA mibovu
Nadhani zitto yupo sahihi hata kama anatumia kujiinua kisiasa ila ni bora aseme ili wenye nchi wajue kama wanapigwa kupitia MIKATABA mibovu
Ni muda sahihi sasa serikali hii ya hapa kazi ya chama cha ccm I angalie hii MIKATABA.. Iwe wazi kwenye hili swala na huko mpaka kwenye madini
 
Huyu Prof. Mi namchukia. Kuwa prof. basi anafikiri anajua kila kitu nilimshangaa sana ile anajidai kuwatetea wezi wa escrow lakini nashukuru Tundu lisu alimtumbua jipu kwa hoja nzito na utetezi wake wa kipumbavu dhidi ya wezi wa escrow
 
Huyu muhongo nae afunge mdomo wake tu, naona anazidi kulipaka mafuta jipu lake lionekane liko tayari kwa kutumbuliwa.
 
Sasa kama anakiri kwa kinywa chake kuwa mikataba mingi ya makampuni ya kuzalisha umeme na ile ya madini ni mibovu, kachukua hatua zipi kama waziri mwenye dhamana kuifuta au kumshauri boss wake kuifuta? Au ndio ile ya viongozi na wanaonyonywa kulalamika pasi na kuwa na upande wenye maamuzi kuchukua hatua? Aina hii ya uongozi wa awamu iliyopita isiambukizwe awamu hii kama vipi ajitumbue kwa kushindwa kazi.
 
Haya sasa leo Magufuli kasema IPTL ni jipu na hatakubali kwenye utawala wake,sasa huyu Muhongo ataweka wapi sura yake?
 
Jana Profesa Muhongo kamshambulia Zito kuhusu IPTL, ni kama alikuwa anaonyesha kama vile Zito alikuwa na maslahi binafsi juu ya IPTL. Alienda mbali zaidi kwa kumshangaa mbunge huyo kwa kitendo chake achodai ni kushikilia hoja ya IPTL kila siku badala ya kutamaza mikataba yote ya Makampuni ya umeme ambayo inauzia umeme Tanesco ambayo amekili ni mibovu na akasema "huyu mtu anaugomvi tu na hii kampuni na anaitumia kwa ajili ya kujijenga kisiasa,maana kila siku yeye na IPTL tu.."


Cha kushangaza leo hii Rais Magufuli amesema kuwa IPTL ni mkataba wa hovyo na Serikali yake hautaendelea nao, meyasema hayo wakati akizindua ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa Megawati 240 cha Kinyerezi II Dar leo.

Mtumbua majipu unasubiri nini hilo ni jipu na limeshaiva
 
IPTL ni ya nani?Watuambie.Na kwanini anaitetea??Anamaslahi gani huko??
 
Kwenye hili zitto yuko sahihi mzee wa majigambo pr mhongo aache kutetea uozo huu kwann kama mikataba ni mibovu isifumuliwe tuanze upya IPTL siyo inaiumiza serikali hata ss wananchi tunaumia kuona tunakazana kulipa kodi ili wengine huduma ziwafikie harafu wakina EL na swahiba wake jk wanaendelea kutuumiza kupitia IPTL
 
IPTL ni ya nani?Watuambie.Na kwanini anaitetea??Anamaslahi gani huko??
Mzee wa deal, unakumbuka hata flow meter za mafuta kule bandarini aliagiza zitumike siku moja kabla Mh Majaliwa kwenda? Na alijua hilo kwa bile alipewa taarifa na ofisi ya PM kwamba kutakuwa na hiyo ziara. Nashangaa bado JPM anaendelea nae na alienda kinyume na kiapo chake.
 
Utachemka mzee "Chache" alihangaika kwa waganga,kutumia waandishi uchwara pamoja na kuwapa "imprest"..baadhi ya wabunge lakini kaufyata!
 
dah ayo majibu yaprofesa!! kweli elimu ya tz ni hovyo kabisa, hakuna cha elimu ya zamani wala ya sasa, wote ndo walewale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…