Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 337
- 698
Waziri Mkuu Sheikh Hasina ameripotiwa kujiuzulu na kuondoka katika mji mkuu wa Dhaka wakati kukiwa na maandamano makali ya kumtaka ajiuzulu
Uamuzi huo umekuja ikiwa ni muda mfupi tangu Umoja wa Mataifa uitake serikali kusitisha mara moja machafuko yanayoendelea nchini humo ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 200, wakiwemo maafisa wa Polisi.
-------
Umoja wa Mataifa umeitaka Serikali ya Bangladesh kumaliza machafuko yaliyosababisha vifo vya raia zaidi 90, wakiwemo polisi 13, kufuatia vurugu za Agosti 4, 2024.
Maandamano hayo yalianza Julai 2024 juu ya malalamiko kuhusu mgawo wa nafasi za kazi Serikalini na kutaka Waziri Mkuu Sheikh Hasina ajiuzulu.
Ghasia hizo zimepelekea takriban watu 11,000 kuwekwa jela, huku shule na vyuo vikifungwa na upatikanaji wa huduma za intaneti kuzuiwa toka Julai 2024.
Soma pia: Maandamano ya Bangladesh yalivyogeuka kuwa mauti, takribani Watu 150 wauawa