I am not a half empty glass kind of a believer or pessimist if you like, I am just a skeptical and curious citizen with a lot of questions in my head.Hivi huo mpango wa kugawa 10% kwa vijana na wanawake sio mkakati wa kununua kura kwaajili ya mwaka 2020 kweli?Hizi ni politically driven policies ambazo zitakuja kuwaletea maumivu makubwa Watanzania,tutarajie inflation kwenda juu kwa kasi ya kimbunga, tutarajie kodi nyingi za ajabu kuanzishwa au kodi kuongezwa ili kugharamia mipango hii, Wakurugenzi kwa kushirikiana na watumishi wengine wa Manispaa wataongeza usumbufu kwa raia ili tu kuhakikisha wanapata fedha ili kukidhi matarajio na matakwa ya serikali.Kiuchumi sijui kama hiyo ni right investment kwani watu wanaopewa mikopo hiyo wengi wao hawana entrepreneurial knowledge ya kuendesha biashara, watapata hiyo mikopo,wataanzisha biashara kisha wafunge biashara zao baada ya miezi kadhaa, sasa sijui lengo la kuanzisha sera za namna hii ni nini hasa,maana kiuchumi naona mafanikio yake yakiwa ni kidogo, labda kama lengo la sera hii ni kuwa_hold potential voters hostage, maana hii kitu kisiasa imekaa vizuri sana, inalipa sana (it pays off) ila kiuchumi ni sawa na time bomb, it can explode any time. Mugabe aliitumia kule Zimbabwe na ilimlipa sana kisiasa ila alikuja kuona majanga yake baadaye,the land confiscation and redistribution program, akaja kuwagawia mashamba Wazimbabwe ambao hawakuwa na maarifa wala utaalamu wa kuendesha kilimo kwa njia za kisasa matokeo yake kilimo kilikuja kuwashinda na nchi kutumbukia ktk dhiki Kubwa ya njaa.Mwanzoni Wazimbabwe walimshangalia kama shujaa kufuatia mpango wake huo wa kuyataifisha mashamba kutoka kwa raia wa Kizungu na kuwagawia Waafrika,na katika uchaguzi alikuwa akishinda kwa kishindo, lakini sasa mambo yamemgeukia, Wazimbabwe wameanza kupata maumivu kutokana na sera zake za kiuchumi.
I fear this situation might happen in Tanzania, populist policies will hurt the economy.