Waziri mkuu Majaliwa: Michango ya wadau waliojitolea kwenye tukio la maporomoko ya tope Hanang ilikidhi mahitaji ya kujenga nyumba

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
536
1,265
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema michango ya wadau waliojitolea kwenye tukio la maporomoko ya tope ilikidhi mahitaji ya kujenga nyumba zote za wahitaji 109 za waathirika wa maporomoko hayo ambayo yalipelekea vifo vya watu 89.

Nyumba hizo ambazo zimejengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) zipo katika kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Soma Pia: -
Ikumbukwe tukio la maafa ya maporomoko ya tope Hanang mkoa wa Manyara yalitokea Desemba 3.2023

 
Back
Top Bottom