Waziri Mkuu apiga marufuku matumizi ya Shisha nchini

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,969
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya shisha na kulitaka Jeshi la Polisi kufuatilia kutokomeza matumizi hayo ili kuwaokoa vijana.

Ameongeza kusema kuwa shisha ni aina ya tumbaku inayokuwa na ina mchanganyiko wa vilevi mbalimbali kama gongo na viroba na mtumiaji anapotumia kilevi hicho hukosa nguvu na hutaka kutumia kila siku na kufuata popote.

 
Hehehe hii serikali kwa style hii watakuingilia hadi chumbani wakupangie siku za kulala na mke wako.

Kweli tumekosa priorities, kila kitu mtu anajisikia leo kesho anatangaza hata ambavyo sio vya msingi, kila mwenye cheo sasa hivi neno lake ndio sheria.

Kazi ipo, nguvu kazi ya taifa ipi inaangamia kwa uvutaji wa shisha? hehehe wanaovuta wenyewe wa kuhesabu tena wengi utakuta ni wenye pesa.

Walianza pool, sasa shisha, sigara wamesema mtu avute private kwa kua zinawaingizia pesa, mara mia wangekomaa na watumiaji wa madawa ya kulevya, wakianza na wasanii wa bongo fleva.
 
https://www.facebook.com/
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya Shisha nchini.

Amesema uvutaji wa shisha una madhara makubwa kwa binadamu, amesema kwa sasa vijana wengi ndio waathirika wakubwa.

Amesema hayo wakati wa hafla ya kufturu iliyoandaliwa na waislamu wa madhehebu ya Shia nchini.
 
Yaan hii nchi ni ya kipumbavuuuu madawa ya kulevya sio ishu tena
Yaani kabisa na tai yangu na suti yangu naacha changamoto zote za wananchi wangu nakaa mbele ya Camera nazungumzia shisha?!
Hivi shisha ina percentage ngapi ya madhara ya kiuchumi na kijamii kwa mamilioni ya vijana wa Tanzania?
Hili ndilo tatizo kubwa kabisa kwa vijana kuliko mengine?
Huu mchezo wenu wa kutusahaulisha madai yetu ya msingi kwenu viongozi tumeugundua.
Shisha waachieni wazazi watashughulika nao,vipi ajira?Vipi ile mikopo?Vipi ubora wa elimu?Vipi pembejeo?vipi uhaba wa waalimu?Vipi thamani ya shilingi?Vipi afya?Vipi michezo?
Kuna mambo ya msingi hatutayasahau,nyie zungukeni wee,mkija tutawauliza haya haya,hakuna cha shisha wala shushu hapa!
Ngoja nilog off watu hawa wanatia hasira kweli!
 
Kuna vitoto vitaumia sana na Sheria hii, Pale slipway ndo kijiwe Chao tena ukitazama vingi viko under 18 vitoto vidogo vya kike, safi sana PM
Hujakosea mkuu. Kama hivyo hapo juu tayari vimenasa na hii ban
 
Shia and Shisha something is go in on!
 
Nawashauri wanajf wenzangu,tukiona hawa jamaa wanataka kutusahaulisha,wanapoleta hizi habari zao sisi hapo hapo tuwakumbushe ya kwetu na mimi kwa mfano naanza hapa.

WAHESHIMIWA AHSANTE KWA CONCERN YENU KUHUSU SHISHA,VIPI NA ILE AHADI YA TATIZO LA MAJI KUISHA DAR?LILE BOMBA JIPYA BADO?
 
Watanzania kuwaelewa ni kazi ngumu sana Makonda alipo Sema hivo kuhusu shiha mkasema anaropoka leo PM kaunga mkono hoja na watanzania hao hao wanampongeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…