Waziri Mkuu akagua athari za Mvua Lindi, atoa maelekezo kwa Mameneja wa TANROADS nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,907
1,340
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) wote nchini kuhakikisha wanakagua vipenyo vya makalvati na madaraja yote katika maeneo yao kabla na baada ya msimu wa mvua ili kujiridhisha kama vinapitisha maji kwa urahisi bila kuathiri barabara.

WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.48 (1).jpeg
Majaliwa ametoa maelekezo hayo leo Aprili 16, 2025 mara baada ya kuwasili mkoani Lindi na kukagua miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoathiriwa na mvua ambapo ameridhishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Timu ya Watalaam kutoka Wizara ya Ujenzi na TANROADS ya kuhakikisha mawasiliano ya barabara yanarejea katika hali yake ya kawaida.

“Kila Meneja wa TANROADS ni wajibu wake ahakikishe makalvati na madaraja yote yanakaguliwa ili vipenyo vilivyowekwa vipitishe maji kwa urahisi, Hivyo fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya ukaguzi wa madaraja na makalvati zitumike kwa kazi hiyo”, amesisitiza Majaliwa.

Aidha, Majaliwa ameelekeza Meneja wa TANROADS mkoa wa Lindi pamoja na timu yake kuweka kambi katika maeneo yaliyopata athari za mvua kwenye barabara hiyo ili kuhakikisha barabara zinakuwa salama na kutoa msaada endapo changamoto yoyote itakapojitokeza kwa uharaka.

WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.48.jpeg
Waziri Mkuu Majaliwa amefafanua kuwa barabara ya Dar es Salaam - Lindi imeharibika katika maeneo mbalimbali yenye madaraja na makalvati kutokana na wingi wa maji unaosababishwa na mvua zinazonyesha mkoani Morogoro yakipitia Mbuga ya Seluous kuelekea baharini.

Halikadhalika, Waziri Mkuu ametoa salamu za pole kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wote wa Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma waliopata kadhia ya kukwama katika barabara hiyo na kueleza kuwa Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma za usafiri na usafirishaji hazikwami katika barabara zote nchini.

WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.47 (1).jpeg
Vilevile, Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wakandarasi pamoja na kutoa taarifa za maeneo yanayopata changamoto kwa vyombo husika ili yaweze kutatuliwa kwa uharaka kwa kuwa Serikali ipo kazini usiku na mchana katika kuhakikisha hakuna kinachokwama.

Majaliwa ameeleza kuwa Mpango wa Serikali ni kuhakikisha hatua kwa hatua inaijenga upya barabara hiyo kwa kiwango cha lami kuanzia Dar es Salaam hadi Mnazi Mmoja mkoani Lindi.

WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.50 (1).jpeg
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameeleza kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 130 kimeidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa madaraja mbalimbali katika Mkoa wa Lindi.

Ulega amefafanua kuwa ujenzi wa daraja la Somanga Mtama (M 60) linatekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya M/S Hunan Construction Enginering kwa gharama ya shilingi Bilioni 12 ambapo tayari Mkandarasi huyo ameshalipwa Shilingi Bilioni 4.1 sawa na asilimia 36.

WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.49.jpeg
 

Attachments

  • WAZIRI MKUU AKAGUA ATHARI LINDI, ATOA MAELEKEZO KWA MAMENEJA WA TANROADS NCHINI.MP4
    80.9 MB
  • WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.47.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.47.jpeg
    472.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.50.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.50.jpeg
    339.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.51.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.51.jpeg
    235.2 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.52.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.52.jpeg
    575.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.52 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.52 (1).jpeg
    355.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.53.jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.53.jpeg
    250.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.53 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-04-16 at 14.59.53 (1).jpeg
    578.1 KB · Views: 1
Uhuni mtupu,tangu mvua za mwaka jana miundombinu iliharibika hakuna aliyehaingaika na ujenzi wa madaraja,sahivi napo wameshituka baada ya mafuriko kupita tena,utashangaa mvua zikiisha wakayaacha makaravati hivyo hivyo yukutane tena mwakani yani ni full maigizo inakera sana.
 
Back
Top Bottom