Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,779
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam, Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amewaondoa wasiwasi watanzania rasilimali za nchi ziko salama kabisa, zile habari zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ni uzushi
Namnukuu
“Taarifa ile ambayo ilisambaa kwenye mitandao ambayo hoja kubwa ilikuwa inaletwa pale kwamba tumechukua mkopo wa dola bilioni 2.5 takribani Shilingi za Kitanzania trilioni 6 au 7 na kwa kubadilishana na kuwagawia bahari na madini yetu, sasa na mimi nitoe changamoto kwa waandishi wa habari mkisoma hizi habari sifa mojawapo ya uandishi wa habari ni kuamiliana kwa kina na taarifa unayoipokea. Kwanza huu siyo mkopo wa kwanza ambao tunaupokea kutoka Mataifa mbalimbali hapa duniani, ninadhani kila siku mnamsikia Mheshimiwa Waziri wa Fedha akisema bungeni kwamba nchi yetu imeshakopa ‘matrilioni’ mangapi, huu siyo wa mara ya kwanza, hakuna mkopo hata mmoja ambao tumewahi kupokea kwa maana ya kuweka rehani rasilimali mojawapo hasa rasilimali za asili, haupo. Lakini pili siyo mkopo wa kwanza kuupokea kutoka Korea, kiukweli katika muundo wa makubaliano yetu huu ni wa pili na katika hizi bilioni 2.5, bilioni 1 ni mabaki yamebaki kule na kuingia kwenye mpango wa pili”
Akaendelea kutolea ufafanuzi...
“Lakini tulichosema hapa muhimu ni kwamba kwanza kukopa ni muhimu kwa sababu ni moja ya nyenzo za kupata mtaji, ni moja ya namna ya kujenga uwezo wa serikali wa kutoa huduma kwa wananchi wake na ni nyenzo ya kujenga uchumi wetu, muhimu ni kwamba moja mnakopa kupeleka wapi na kwa masharti gani? Na tumeweka wazi masharti ambayo tunayo sisi kama nchi tumeshajiwekea utaratibu kwenye sera zetu za kifedha, namba moja ni kutumia kadiri iwezekanavyo mapato ya ndani, ndiyo maana tunapambana kuongeza uwezo wa ndani kwa maana ya mapato kupitia kodi za Watanzania na ndiyo maana kila siku tunapandisha, la pili inapokuja kwenye suala la kupokea mikopo na misaada kipaumbele cha Tanzania ni kuchukua mikopo ambayo si ya kibiashara kwa maana ya commercial loans ambayo moja; ina riba ndefu sana lakini muda wa kulipa ni mfupi, kwa hiyo sisi kipaumbele chetu ni kuchukua mikopo yenye masharti nafuu. Lakini tatu kipaumbele chetu tukishachukua mikopo hii inakwenda wapi? Tunachukua mikopo kwa ajili ya kwenda kwenye sekta za uzalishaji na kujenga uwezo wa nchi, kwa hiyo hatukopi kwa mfano kwa ajili ya matumizi ya kuanza kununua magari, tuanze kulipana mishahara, hapana, tunakopa kwenda kwenye sekta za uzalishaji ndiyo maana katika ule mkopo wa kwanza tulijenga hospitali ya Mloganzila, tukajenga daraja la Tanzanite”- Prof. Kitila Mkumbo.
Mwisho.
Pia soma