Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,201
- 5,585
Waziri Mchengerwa akiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva Bodaboda na bajaji wa Jiji la Dar es Salaam. Waziri huyo ameonekana kuwatambua madereva bodaboda na bajaji kama Maafisa usafirishaji.
Akigusia hoja hiyo Mchengrwa alisema:
“Kuanzia sasa sitaki kusikia kamata kamata ya hovyo, inayotokana na wakati fulani kuwepo na sintofahamu baina yenu na Maafisa wa Serikali, mchango wenu ni mkubwa sana hivyo Serikali ya Chama cha Mapinduzi inawathamini sana ninyi Maafisa usafirishaji wa bodaboda na bajaji, na ndio maana ninataka kuona ushirikiano mzuri unakuwepo baina yenu na Serikali".
Nini mtazamo wako kuhusu hoja hii?
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Sare za bodaboda kuwekwa picha ya Rais Samia na Mchengerwa kuagiza madereva bodaboda waache kusumbuliwa halitaongeza uvunjifu wa sheria?
- Kuelekea 2025 - Mchengerwa: Wakuu wa Mikoa wote simamieni mfumo wa Kidijitali wa kuwatambua Madereva Bodaboda na Bajaji