Waziri Mchengerwa asisitiza watumishi kubadili utendaji kazi

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
168
116
Watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), wametakiwa wabadilike katika utendaji wao na wasiishi kwa mazoea ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Septemba 5, 2023 na Waziri wa (TAMISEMI), Mhe.Mohammed Omary Mchengerwa wakati akichangia Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Jason Rweikiza kuhusu matokeo ya uchambuzi wa sheria ndogo, ambapo amefafanua kuwa tayari Serikali imeshatoa fedha nyingi katika miradi mbalimbali kilichobaki ni kufanya usimamizi madhubuti.

Sheria hizo zilizowasilishwa Bungeni katika Mkutano wa 10 Septemba 20, 2022 na Mkutano wa 11 wa Bunge Novemba 7, 2022.

Pia taarifa hiyo imetoa matokeo ya uchambuzi wa taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu dosari na hitilafu za sheria ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na Mkutano wa Tisa wa Bunge.

“Tumepokea mapendekezo ya Kamati, naomba watumishi wenzangu tuache utendaji wa kimazoea, “ amesema na kuhakikisha kuwa sheria na kanuni vitaendana na Katiba.

Pia amesema atahakikisha sheria na kanuni mbalimbali zinaboreshwa ili kulinda, kutetea maslahi ya wananchi.

Mapema jana baada ya kuwasili katika Ofisi yake mpya mtumba Mhe. Mchengerwa alisisitiza mambo makuu manne katika utendaji wa kazi.

Mambo hayo ni pamoja na viongozi ( ma RC na Ma DC) kushuka chini kwa wananchi, Wakurugenzi wote kuhakikisha kumaliza miradi katika kipindi walichopanga, kuondokana na rushwa pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

IMG-20230905-WA0020.jpg
 
Ndio sasahivi najua kwamba bunge lipo on session kweli hili bunge ni la wapuuzi.
 
Huyu ni Mkwe wa Mama Mkubwa,ebullient tuwe wastaarabu kidogo wakati wa kumjadili.
 
Mkwe wa taifa ushasema sisi ninani tupinge hilo?? Unaamishwa amishwa Kila wizara mradi tu upige mahela...
 
Back
Top Bottom