JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,640
- 6,315
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni ameulizwa juu ya kufungiwa kwa Kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe maarufu kwa jina la Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza Kwa Lulenge, amesema rufaa ya kufungiwa kwa kanisa hilo haijafika mezani kwake, hivyo hawezi kuzungumza kwa urefu.
Barua ya kufungiwa kwa kanisa hilo ya Julai 25, 2024 iliyotolewa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia imetaja sababu za kulifunga Kanisa hilo ni kwenda kinyume cha taratibu za usajili ikiwemo kuweka kutoza Tsh. 500,000 kupata huduma ya maombezi tofauti na Imani ya Kikristo na kinyume na Katiba pamoja na Kanuni za Kanisa lako, zinazotambuliwa rasmi na Ofisi ya Msajili wa Jumuiya.
Mengine ni kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni.
Kutoa mahubiri chonganishi
Kuhamasisha waumini wa kanisa lake (Mchungaji Domique) kuua watu kwa dhana au tuhuma za uchawi/ushirikina.
Kutokana na hali hiyo, kwa barua hii, unajulishwa kuwa unatakiwa kufunga mara moja shughuli na huduma zote zinazotolewa katika Kanisa linaloendeshwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe maarufu kwa jina la Kiboko ya Wachawi wakati taratibu nyingine za kisheria dhidi ya Kanisa la Christian Life Church zikiendelea. Utekelezaji wa maelekezo haya ufanyike kabla ya tarehe 28/07/2024.
Pia soma
~ Kufungiwa kwa kanisa la “Kiboko ya Wachawi” pongezi kwa Serikali
~ Waumini wa Mchungaji Domique Kashoix Dibwe, maarufu 'Kiboko ya Wachawi' wafurika Kanisani kusubiri ibada hata baada ya kanisa kufungwa
~ Serikali chukueni hatua za dharura na haraka dhidi ya Kiboko ya Wachawi kinachoendelea hapa buza mtalaumiwa
~ Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"