Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 45,440
- 64,241
Nchi hii inakabiliwa na hali mbaya sana ya uharibifu mkubwa mno wa mazingira unaotokana na kukata miti kwa ajili ya biashara mbaya ya mkaa na kuni. Kulima kwenye vyanzo vya maji nitazungumzia wakati mwingine.
Waziri, maeneo ya kanda ya ziwa uliyotembelea ndio kitovu cha biashara ya mkaa. Tabora, Shinyanga na Simiyu miti inakatwa haswa na mkaa unazalishwa na kuuuzwa bei rahisi sana, Unaweza kupata gunia la mkaa kwa Sh.15,000/=! kwenye hii mikoa. Kila kukicha hii mikoa inazidi kugeuka jangwa. Hii iwe alama nyekundu ya hatari.
Nilikusikia unamuambia mama mmoja uliyekuwa unampa jiko la gesi kwamba aachane na kuni kwa sababu zinazalisha sumu. Nataka niamini ukweli halisi wa moyoni mwako ni kwamba unauona mkaa ni uharibifu wa mazingira na ulifanya hivyo tu kwa yule mama ili kupunguza maneno kutoka kwa wakosoaji wa chama chako ambao kama ungesema mkaa na kuni ni janga kwa mazingira wangesema chama chako mmekuwa madarakani muda wote tangu kupata uhuru lakini mmeshindwa kuumaliza umaskini wa hao watu wanaotegemea mkaa.
Jambo la kushangaza, ni kwamba hata hata watu wa daraja la kati kiuchumi na matajiri wanaoishi mijini bado wanatumia sana mkaa na kuni. Watakuwa na jiko lao la gesi kwa ajili ya kupikia mama mwenye nyumba akiwepo na pia sio kwa vyakula vyote. Dada wa kazi inabidi apikie mkaa/kuni. Maharage, nyama, makande, wali, ugali mara nyingi vinapikiwa kwenye mkaa au kuni. Hawa hata umeme wa JHNPP ukianza kupatikana wataendelea tu na matumizi yao ya mkaa kama wasipodhibitiwa.
Mh Waziri, shirikiana na mawziri wengine kupandisha sana gharama za mkaa kwa kodi urasimu na vibali vya biashara mpaka watu wa mjini wauone mkaa kama anasa na waukimbie, halafu fanyeni bei na upatikanaji wa gesi uwe rahisi kwa njia hizo hizo.