Salam Jf,
Hapa wilayani Hai mkoani kilimanjaro idara ya ardhi inanyanyasa sana wananchi. Unakuta mtu umeomba hati toka mwaka 2000 mpaka leo hati haijatoka na taratibu zote umekamilisha.
Kibaya zaidi ukienda kulalamika kwa afisa ardhi wa wilaya anakujibu kwa dharau na kejeli utadhani yeye ni Mungu mtu.
Bad enough yupo kuuza open space kila kona ya mji wa bomang'ombe. Mheshimiwa Waziri naomba ufuatilie kilio cha wana Hai tunanyanyaswa sana na huyu afisa ardhi wa wilaya