Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,330
- 4,692
Waziri ardhi, William Lukuvi leo tarehe 16 Februari 2021 amefika fukwe za Coco Beach akakuta kuna ujenzi unaendelea.
Akaagiza kusimamishwa kwa ujenzi na kubomolewa kwa uzio huo kwa kua fukwe za Coco beach ni bure.
Waziri wa ardhi, William Lukuvi amefika kwenye fukwe za Coco Beach na kukuta ujenzi wa kiwanja ukiwa unaendelea kinyume na sheria, "niulize nani kawambia mjenge viwanja vya watu watano watano hapa au ni wazo lenu?
Kwa sababu kama ni interest ya michezo nyinyi mna viwanja vingi, Kinondoni kuna viwanja vingi kila shule ya sekondari ina kiwanja cha michezo sasa kwa nini hapa"?
Waziri Lukuvi aliamua kusitisha na kutoa agizo la kuvunja leo ujenzi huo unaondelea.
Pia Waziri Lukuvi amewapa onyo Meya na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kutokua na tamaa ya maeneo ya wazi ambayo ni mali ya Umma.
=========
Rais amesema fukwe zitumike kwa wananchi wote huru.
Hakukuwa na sababu yoyote, Mkurugenzi. Hamna kiu ya viwanja vya michezo Dar es Salaam. Kama mnataka ku-develop viwanja vya michezo si lazima muingie kwenye open space hii ya thamani. Hawa wote wanaokaa hapa wana ma-gym, wana hela ya kwenda gym.
Hivi mkilitunza hili eneo likakaa likatunzika, likaboreka tukapanga eneo hili lote pamoja tukimaliza infranstructure; mna hasara gani, mna haraka gani?
Huyu ni Breweries kweli aliyechagua kwamnba anataka hapa? Kwanini msimchagulie mahala pengine? Wha kila mara mupo hapa? Why Coco Beach? Likikaa hivi linawakera?
Hili wazo lazima lina mtu mmoja. Meya, hili eneo linawakera likiwa wazi? Viwanja vipo vinne hivi; vimewashinda. Kuanzia leo nitavichukua nitatoa hati itaandikwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, maana nyie mmeshindwa ku-manage. Mna tamaa.
Unajenga uwanja wa watu watano alafu unasema eti utawasaidia watu?
Open space zote Mkurugenzi nikukumbushe, zinatawaliwa na sheria. Nimeshauliza majirani wote, hawakushirikishwa. Matumizi yoyote ya open space yanapobadilishwa lazima yashirikishe wadau majirani. La pili, Afisa Mipango Miji umewadanganya; haiwezi kuwa temporary structure hii, ya manondo! Huwezi kutia ndondo hapa ukasema ni temporary structure. Hili ni jengo la kudumu.
Kwanza mmekiuka Sheria, hamkushirikisha wadau. Hatukukuta mabango yoyote hapa mulipoandika kuwa eneo hili tunataka tuliwekee matumizi haya ya kudumu. Lakini tunabadilisha matumizi, sasa tumeamua wananchi huku Coco Beach tunataka tuwajengee uwanja wa kucheza watu watano watano. Hamkufanya!
Lakini upo mwongozo. Ninyi Halmashauri za wilaya uwezo wenu ni wa kupanga tu open space lakini si kuzibadilisha matumizi hamuwezi mpaka mushirikishe Wizara.
Na ninarudia tena, kote! Makamishna wasaidizi mikoa yote ndiyo maana nimewaweka; hakuna halmashauri yoyote kubadilisha matumizi ya Open space. Mpaka ninyi ofisi zangu za mikoa zilizopo kule chini ya Makamishna Wasaidizi mjue.
Ninawataka Makamishna Wasaidizi wapekue hizi Open space. zinazotamaniwa tamaniwa namna hii. Lazima zirudi kama Open space.
Mkishapanga ninyi wapangaji kuwa hii ni open space, inatoka mikononi mwenu na kuwa mali ya wananchi. Kwahiyo munapotaka kubadilisha si kazi yenu, lazima wananchi waulizwe. Hamuwezi kukaa kule mmejifungia alafu mnapora ardhi yote ya watu wa Dar es Salaam alafu munatengeneza kitu cha watu watano.
Ni marufuku kwa watu wangu kuwashauri vibaya Wakurugenzi kubadilisha Masterplan. Masterplan hamna uwezo wa kubadilisha. Ninyi mna uwezo wa kuzipanga tu. Zibaki kama zilivyo!
Hapa mtaendelea kupatunza kama palivyo, mtapasafisha na wananchi wataendelea kushughulika kama palivyo. Na tulisema kama Serikali tutashirikiana na wadau wenye jiji hili la Dar es Salaam tupange pamoja matumizi bora zaidi endelevu ya eneo hili la Coco Beach.