chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,225
- 27,382
Tangu Jamuary Makamba awe Waziri wa Mambo ya Nje, hakika ameonyesha umahiri wake wa kuwapika viongozi. Humphrey Polepole ninayemuona, sio yule wa kipindi cha miaka kadhaa nyuma.
Miaka kadhaa nyuma, Polepole alikuwa anakata mauno kama Nyosh El Saadat wa FM Academia, sasa Boggoss Band. Sasa hafanyi hivyo, ametambua kwamba watanzania wanapenda kiongozi wao awe na staha, aondoe tabia za hovyo hovyo zinazoashiria utoto na ulimbukeni. Hongera sana January Makamba kwa kuwapa uongozi mabalozi wetu hasa Polepole.
Endelea "kumpika" katika mambo ya protocol na utendaji wa serikali. Ametokea katika NGO za mitaani mitaani huko alikiwq anatembea na kibegi cheusi kwapani, na hicho kibegi ndio ilikuwa ofisi yake. Hajajua kwamba kuna mambo lazima yahakikiwe kiserikali kabla ya kuwa rasmi,mfano matumizi ya dawa ambazo yeye anataka zije bila kujali kwamba lazima zihakikiwe na mamlaka za nchi, kuzipima kama hazina madhara, na pia kuwasiliana na WHO.
Na mwisho, hata mazungumzo yake na Jenerali Ulimwengu yalionyesha ukomavu na utulivu wa kiuongozi. Tofauti na zamani ambapo alikiwq mjivuni, mwenye utoto mwingi, anatukana viongozi mitandaoni. Binafsi nilimfananisha na Mdude Nyagali, moja ya vijana wa hovyo wa Chadema.
Kongole January Makamba kwa kazi nzuri, endelea kumsimamia kijana wako Humphrey Polepole.