Waziri Jafo: Wauza nyama Buchani kuna ujanjaujanja wanaufanya kuibia Wateja kwenye mizani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,463
Juni.jpg
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Selemani Jafo amefichua namna wauza nyama buchani wanavyocheza na mizani na kuwaibia wateja wao kwa kuwawekea vipimo visivyo sahihi.

Alibainisha mbinu hizo Julai 12, 2024 alipotembelea kituo cha kupimia ujazo wa malori cha Wakala wa Vipimo (WMA) cha Misugusugu, mkoani Pwani, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake, Exaud Kigahe na Naibu Katibu Mkuu wizarani, Balozi Dk. John Simbachawene.

"Ile mizani ya zamani yenye sufuria upande mmoja na jiwe kwingine kila ukiondoka unakuta kaweka jiwe la ujazo wowote, hawezi kuuacha mzani ukiwa bila jiwe.

"Ukiingia buchani anakuuliza unataka kilo ngapi, ukisema tu anatoa jiwe alilokuwa ameweka anaweka la ujazo unaotaka wewe, ule ni ujanjaujanja tu wa kukuibia.

"Anaweka jiwe muda wote kwa sababu anajua lisipokuwapo mizani haiwezi kuwa sawa, kwahiyo mteja anaweza kushtukia kwa sababu akitoa jiwe tu mzani unaangukia kwenye lile sufuria kubwa upande mwingine. Kwahiyo, unapimiwa kilo moja wakati mwingine robo nzima imeibiwa.

"Sijui kama wenzangu mnayaona haya lakini inawezekana wengine ni wa mboga nane hamjawahi kuishi maisha ya uswahilini, hivyo hamwezi kuelewa hiki ninachosema, lakini ndiyo hali yenyewe," alisema Waziri Jafo.

Alisema wapo baadhi ya wafanyabaishara ambao wamekuwa wanatumia mbinu zingine za kuwaibia wateja ikiwamo ya kukandamiza mizani kwa kutumia kisu, wengine wakitumia sumaku.

Alisema WMA ina kazi kubwa ya kupambana na wizi huo, akiwataka viongozi wake kushirikisha maofisa biashara wa mikoa na wilaya kuwatafuta na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo alielekeza watendaji walio chini yake kumaliza hujuma zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wanaopunguza ujazo wa mifuko ya saruji.

Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu kupungua kwa ujazo wa mifuko hiyo ya saruji ambayo inapotoka kiwandani inakuwa na ujazo sahihi wa kilo 50, lakini inafika kwa wateja ikiwa na wastani wa kilo 40 au 45.

"Inawezekana ikawa ni kazi kubwa, lakini sisi ndiyo tumepewa wajibu wa kuhakikisha kunakuwa na vipimo sahihi, mtendaji mkuu na timu yako mnapaswa kusimamia kuhakikisha hujuma hizi zinakomeshwa," aliagiza Waziri Jafo.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Exaud Kigahe alimpongeza Dk. Jafo kwa kuanza kazi kwa kasi baada ya kuapishwa hivi karibuni na kumwahidi kuwa atampa ushirikiano katika utendaji kazi wake.

Alisema taasisi nyingi zilizo chini ya wizara hiyo zinafanya kazi ya kuweka mazingira mazuri ya wenye viwanda na biashara kustawi na kulinda ushindani kwenye biashara na walaji wa mwisho ili wanaouza wasiibiwe na wale wanaonunua wasiibiwe.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla alisema wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na waziri na kuahidi kuyafanyia kazi katika muda uliopangwa.

Kihulla alieleza kuwa WMA kupitia kituo hicho cha Misugusugu, ina uwezo wa kuhakiki mita za umeme, dira za maji na magari yanayotumika kusafirisha vimiminika.

Pia soma ~ Wauzaji wa nyama Mbezi Beach kuna michezo wanafanya kwenye mizani
 
Jafo pengine upo sahihi ,,, lakin mimi naona bwana jafo una - deal na mambo madogo sana ,, haya ungewaachia watendaji wako wa chini ,,, sasa kweli waziri mzima unafuatilia upimaji wa nyama kweli ???
 
Jafo yupo sawa'

Mkubwa akiongea attention ya ufatiliaji inakuwepi
 
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Selemani Jafo amefichua namna wauza nyama buchani wanavyocheza na mizani na kuwaibia wateja wao kwa kuwawekea vipimo visivyo sahihi.

Alibainisha mbinu hizo jana alipotembelea kituo cha kupimia ujazo wa malori cha Wakala wa Vipimo (WMA) cha Misugusugu, mkoani Pwani, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake, Exaud Kigahe na Naibu Katibu Mkuu wizarani, Balozi Dk. John Simbachawene.

"Ile mizani ya zamani yenye sufuria upande mmoja na jiwe kwingine kila ukiondoka unakuta kaweka jiwe la ujazo wowote, hawezi kuuacha mzani ukiwa bila jiwe.

"Ukiingia buchani anakuuliza unataka kilo ngapi, ukisema tu anatoa jiwe alilokuwa ameweka anaweka la ujazo unaotaka wewe, ule ni ujanjaujanja tu wa kukuibia.

"Anaweka jiwe muda wote kwa sababu anajua lisipokuwapo mizani haiwezi kuwa sawa, kwahiyo mteja anaweza kushtukia kwa sababu akitoa jiwe tu mzani unaangukia kwenye lile sufuria kubwa upande mwingine. Kwahiyo, unapimiwa kilo moja wakati mwingine robo nzima imeibiwa.

Pia soma ~ Wauzaji wa nyama Mbezi Beach kuna michezo wanafanya kwenye mizani

Waacheni waibe tu, hata TRA wanawaibia wa mama mboga mboga mamilioni na Mmejua mmefanya nini?
 
Sasa ameongea, nia yake ni nini hasa, kutufundisha jinsi ya kuiba kwa kutumia mizani au tumuone kuwa na yeye ni mtoto wa mjini ameushutukia ujanja huo! Amemaliza kuongea na sisi huku mitaani tunaendelea na wizi wetu uleule hakuna jipya.
Ameongea utafikir Hana mamlaka.
 
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Selemani Jafo amefichua namna wauza nyama buchani wanavyocheza na mizani na kuwaibia wateja wao kwa kuwawekea vipimo visivyo sahihi.

Alibainisha mbinu hizo Julai 12, 2024 alipotembelea kituo cha kupimia ujazo wa malori cha Wakala wa Vipimo (WMA) cha Misugusugu, mkoani Pwani, akiwa ameambatana na Naibu Waziri wake, Exaud Kigahe na Naibu Katibu Mkuu wizarani, Balozi Dk. John Simbachawene.

"Ile mizani ya zamani yenye sufuria upande mmoja na jiwe kwingine kila ukiondoka unakuta kaweka jiwe la ujazo wowote, hawezi kuuacha mzani ukiwa bila jiwe.

"Ukiingia buchani anakuuliza unataka kilo ngapi, ukisema tu anatoa jiwe alilokuwa ameweka anaweka la ujazo unaotaka wewe, ule ni ujanjaujanja tu wa kukuibia.

"Anaweka jiwe muda wote kwa sababu anajua lisipokuwapo mizani haiwezi kuwa sawa, kwahiyo mteja anaweza kushtukia kwa sababu akitoa jiwe tu mzani unaangukia kwenye lile sufuria kubwa upande mwingine. Kwahiyo, unapimiwa kilo moja wakati mwingine robo nzima imeibiwa.

"Sijui kama wenzangu mnayaona haya lakini inawezekana wengine ni wa mboga nane hamjawahi kuishi maisha ya uswahilini, hivyo hamwezi kuelewa hiki ninachosema, lakini ndiyo hali yenyewe," alisema Waziri Jafo.

Alisema wapo baadhi ya wafanyabaishara ambao wamekuwa wanatumia mbinu zingine za kuwaibia wateja ikiwamo ya kukandamiza mizani kwa kutumia kisu, wengine wakitumia sumaku.

Alisema WMA ina kazi kubwa ya kupambana na wizi huo, akiwataka viongozi wake kushirikisha maofisa biashara wa mikoa na wilaya kuwatafuta na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo alielekeza watendaji walio chini yake kumaliza hujuma zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wanaopunguza ujazo wa mifuko ya saruji.

Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu kupungua kwa ujazo wa mifuko hiyo ya saruji ambayo inapotoka kiwandani inakuwa na ujazo sahihi wa kilo 50, lakini inafika kwa wateja ikiwa na wastani wa kilo 40 au 45.

"Inawezekana ikawa ni kazi kubwa, lakini sisi ndiyo tumepewa wajibu wa kuhakikisha kunakuwa na vipimo sahihi, mtendaji mkuu na timu yako mnapaswa kusimamia kuhakikisha hujuma hizi zinakomeshwa," aliagiza Waziri Jafo.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Exaud Kigahe alimpongeza Dk. Jafo kwa kuanza kazi kwa kasi baada ya kuapishwa hivi karibuni na kumwahidi kuwa atampa ushirikiano katika utendaji kazi wake.

Alisema taasisi nyingi zilizo chini ya wizara hiyo zinafanya kazi ya kuweka mazingira mazuri ya wenye viwanda na biashara kustawi na kulinda ushindani kwenye biashara na walaji wa mwisho ili wanaouza wasiibiwe na wale wanaonunua wasiibiwe.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla alisema wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na waziri na kuahidi kuyafanyia kazi katika muda uliopangwa.

Kihulla alieleza kuwa WMA kupitia kituo hicho cha Misugusugu, ina uwezo wa kuhakiki mita za umeme, dira za maji na magari yanayotumika kusafirisha vimiminika.

Pia soma ~ Wauzaji wa nyama Mbezi Beach kuna michezo wanafanya kwenye mizani

Hii ni kweli
 
Kama halmshauri waziri mkuu anakuja kuibua wameiba mamilion kadhaaa na awajapelekwa ndan wao nani wasituibie tule kwaa urefuu wakamba zetu tu
 
Ng'ombe bei ghali sana,ndo maana watu wanafanya ujanja

vIng'ombe vyetu baada ya kuchinjwa kanabakiza kilo 100 na wakati huo umekanunua laki 8,bei ya nyama kilo 8000
 
Back
Top Bottom