KERO Waziri Dorothy Gwajima, tunaomba umwangalie huyu Sheikh na Mahubiri na Mada zake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sio tu serikali inaweza kujua matatizo yote kupitia kwenye mitandao ya jamii ila nimekutana na huyu anajiita sheik zaid makubul kuhusu maada za kibaguzi na makabari.

Kwako waziri Doroth gwajima kupitia wizara yako unaweza kumpa onyo kali mfano wa watu hawa wanaweza kusababisha makabila kutoelewana tena upande wa ustwai wa jamii.

Mada yake

View: https://www.youtube.com/watch?v=9Be9zcMEsag
 
Ndio maana inatakiwa viongozi wa dini wawe wamesoma
Kweli kabisa Mkuu,tatizo watu wengi wa Pwani hawapendi elimu,kwa Zenji kuna vyuo vya Dini na wanasoma vizuri tu,sasa ishu ipo Pwani.Sijui kama Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro kinatoa kozi za Dini..siku 1 kuna Shehe mmoja aliwaambia waumini wasisherehekee X-Mas na Mwaka Mpya kwa sababu ni Sikukuu za Wakristo na Wayahudi. Kwani Wakristo wote wanaamini X-mas,sio wote,pia Wayahudi na X-mas wapi na wapi,wao wana kalenda yao na wana Sikukuu zao.
 
Sio kila anayevaa kanzu na kofia basi ni Sheikh kasoma ,bali zama hizi wajinga wengi wamejikita jukuma la kuisema dini bila ya Elimu na watu wasiojua wanawaona kuwa Masheikh kumbe ni Masheikh wa mchongo na wapo wengi hapa Tz mfano wakina Dr.Sule , Kipozeo nk
 
Ingekuwa mtu akizaliwa kabila Fulani ,nchi , familia,ukoo , rangi n.k automatically anakuwa na mapungufu hawezi kurekebishika basi kusingekuwa na haja ya dini kupelekwa kwa walimwengu wote bali ingejikita kwa watu Fulani pekee sababu wengine hawezi kubadilika.

Uislamu ubora wa mtu sio kabila ,rangi ,nchi nk bali ni uchamungu wake .
IMG_20240521_100327.png
 
Back
Top Bottom