Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 486
- 707
ZANZIBAR YASHINDA TUZO KUBWA YA UTALII DUNIANI KAMA ENEO BORA KWA MATUKIO BARANI AFRIKA 2024
Zanzibar imeendelea kujidhihirisha kuwa moja ya maeneo bora la utalii duniani baada ya kujinyakulia tuzo maarufu katika "World Travel Awards".
Zanzibar imefanikiwa kupata tuzo ya Eneo Bora kwa Matukio na Matasha Barani Afrika 2024, hatua inayothibitisha ukuaji na umaarufu wa visiwa hivi katika sekta ya utalii. SM Tuzo hiyo ilitangazwa rasmi katika hafla maalum iliyofanyika usiku wa kuamkia, Oktoba 19, 2024, mjini Mombasa, Kenya.
Tuzo za World Travel, ambazo zilianzishwa mwaka 1993, zinalenga kutambua, kutuza, na kusherehekea ubora katika sekta zote muhimu za usafiri, utalii, na ukarimu. Tuzo hizi zinatambulika kimataifa kama alama ya ubora katika sekta ya utalii na maeneo mbalimbali duniani.
Tuzo hii ni ishara ya kuthamini jitihada za Zanzibar katika kuandaa matukio na tamasha za kimataifa huku ikidumisha urithi na utamaduni wake. Pia inaonesha kuwa Zanzibar inazidi kuwa kivutio kikubwa cha kimataifa katika sekta ya utalii na uwekezaji.
Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale pamoja na Kamisheni ya Utalii Zanzibar wanatoa shukrani kwa wadau wote ambao wamechangia kufanikisha ushindi huu.
Tuzo hii ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya sekta za umma na binafsi katika kuimarisha taswira ya Zanzibar kwenye ramani ya dunia kama kivutio cha kipekee.